-->

NDEGE YAPASUKA MATAIRI WAKATI INATUA MKOANI ARUSHA

Nikiwa mmoja wa abiria tuliosafiri na PW kurudi Arusha leo, ndege ya shirika hilo yenye usajili No 5HPWI imepata kizaazaa wakati wa kutua baada ya tairi mojawapo kupasuka kwa kishindo, likufuatiwa na mengine yote ya nyuma ambapo yalipasuka pia na kuacha vipandevipande kwenye njia ya kurukia.

Waliookota vipande hivyo wamesema kuwa wamekuta viraka(pechi, watu wa magari wananielewa zaidi hapa), kitu ambacho si kawaida kwenye usafiri wa jamii hii!

Rubani wa ndege hiyo amejitahidi kuitoa ndege hiyo nje ya njia ili kutozuia ndege nyingine kuruka, japokuwa mwishowe ilimgomea kabisa na kubaki ikisota pembeni mwa njia hiyo.

Kikubwa ni kwamba hakuna madhara yaliyowapata abiria, akiwemo Bwana Lowassa.
 CHANZO:JF
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment