Na mwandishi wetu
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuendeleza michezo nchini ili kuleta ufanisi katika sekta ya michezo.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi mipira 100 kwa timu ya taifa ya vijana chini ya
miaka 17 jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bwana
Sunil Colaso alisema uwekezaji katika michezo ni mhimu hasa katika
kipindi hiki amabacho Tanzania inajipanga kushiriki katika mashindano ya
kikanda na kimataifa.
“Airtel
Tanzania tunakabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya
miaka 17 kama sehemu ya juhudi zetu kusaidia maendeleo ya michezo.
“Tutaendelea
kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha nchi
inapata mabalozi wa kutuwakilisha vizuri katika mashindano ya kimataifa”
alisema
Colaso
alisema mwaka 2011 kampuni yake kwa makusudi ilianzisha Airtel Rising
Stars ikiwa ni mpango wa kuvumubua na kuendeleza vipaji kwa vijana
wadogo kutoka ngazi ya chini ili kuwapeleka ngazi za kimataifa.
Wakati
wa hafla hiyo, mkongwe wa klabu ya Manchester United Andy Cole aliwaasa
vijana hao chini ya miaka 17 kuongeza bidii ili kutimiza ndoto zao za
kucheza kwenye timu kubwa duniani.
“Nimeona
vipaji vingi Tanzania. Wachezaji wanaweza kabisa kuchezea klabu kubwa
kama wataongeza bidii katika mazoezi yao. Naomba nichukue nafasi
kuwakumbusha wachezaji chini ya miaka 17 kuwa na nidhamu si ndani tu ya
uwanja bali na nje ya uwanja kwani hiyo ndio nguzo ya mafanikio”
Alisema.
Nae
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa aliwashukuru kampuni ya Airtel
Tanzania kwa juhudi zake endelevu kusaidia michezo na kutoa wito kwa
makapuni mengine kuiga mfano wa Airtel katika kusaidia michezo
“Tunahitaji
nguvu za pamoja kati ya sekta binafsi na umma kama kweli tunataka
maendeleo katika michezo. Nawashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika
michezo, niwaombe makampuni mengine waige mfano huu katika kusaidia
juhudi za Serikali kuendeleza michezo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala jerry Slaa(kushoto) akimuongoza mchezaji wa zamani wa
Manchester United Andy Cole kwenda kuwafunda vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17. Shughuli hiyo
ilifanyika jana Dar es Salaam katika viwanja vya karume mara baada ya mchezaji
huyo kuzuru/kutembelea ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania. Picha na
mpga picha wetu
Mchezaji
wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) akiwasalimia vijana
chini ya miaka 17 kabla ya kukutana na timu ya vijana wa timu ya Taifa chini ya
miaka 17 katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Meya
wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa. Picha
na mpga picha wetu
Meya
wa manispaa ya Ilala(wa pili kushoto) akikabidhi mipira iliyotolewa na Kampuni
ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania Bwana Jamali Malinzi (kushoto) katika hafla ya makabidhiano
iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni mchezaji wa zamani wa
klabu Manchester UnitedAndy Cole na Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Sunil
Colaso(kulia). Picha na mpga picha wetu
Mchezaji
wa zamani wa klabu ya Manchester united(Kulia) akionyesha ufundi wa kuchezea
mpira mbele ya timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 jana jijini Dar es
Salaam. Anayeangalia ni Meya wa Manispaa ya Ilila Jerry Slaa. Picha na mpga
picha wetu
Mkurugenzi
mtendaji wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso(kushoto) akitoa hotuba fupi mda
mfupi kabla ya kukabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka
17jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kulia ni Mchezaji wa zamani wa Manchester
United Andy Cole na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa(wa pili kushoto).
Picha na mpiga picha wetu
CHANZO:SHAFFIHDAUDA
0 comments :
Post a Comment