GOLIKIPA wa timu ya Yanga, Juma Kaseja amefunguka kuhusu uamuzi wa kutompa mkono golikipa wa timu ya Simba Ivo Mapunda, kwenye mechi ya hisani ya Nani Mtani Jembe.
Ivo amedai kuwa hana bifu lolote na goli kipa huyo ingawa ni kweli hakumpa mkono, na kwamba yale yalikuwa ni maamuzi tu.
"Unajua kaka watu wanaongea sana lakini mimi sina bifu lolote na Ivo,hivyo ni vitu vya kawaida tu na maamuzi ya mtu." Kaseja ameiambia blog ya Supermariotz.
Simba iliibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Yanga, matokeo yaliyopelekea Yanga kumtimua kocha Mholanzi Ernie Brandts.
0 comments :
Post a Comment