-->

ZITTO KABWE AKANUSHA UVUMI WA YEYE KUWA NA BIFU NA DR. SLAA

"Tatizo la baadhi yetu ni kuishi maisha ya uongo na fitna. Sina tatizo na Dr Slaa. Ni Katibu Mkuu wa chama na amefanya mengi mazuri kufikisha chama hapa.

Sasa hivi watu wanajitahidi sana kuchochea kwa kugeuza maneno ionekane kwamba nina tatizo na Katibu Mkuu wangu. Ziara yangu Kigoma haikuwa 'kumjibu Dr Slaa' kama inavyosemwa. Sina cha kumjibu Katibu Mkuu wangu.

Ninalo jukumu kama mwanachadema kutoa maelezo kuhusu tuhuma dhidi yangu na pia kuongea na wananchi kuhusu matatizo ya nchi yetu. Hayo sio majibu kwa Dr Slaa kwa sababu ni uonevu kusema Dr Slaa ni Kamati Kuu.

Mimi nitaendelea kutumikia wananchi wa Kigoma na watanzania wote kama mwanachadema na Mbunge. Anayesema naidhoofisha Chadema ni muongo na apuuzwe"
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment