Nimesikitishwa sana na jinsi Gazeti la kaka yangu Mbowe (Tanzania Daima) la leo Disemba 20, 2013 lilivyotumia jina langu kutafuta mapato na labda kwa nia nyingine.
Gazeti hilo katika ukurasa wake wa kwanza na wanne linaripoti kwamba jana Disemba 19, 2013 nilikuwa mkoani Mwanza kumuwakilisha Mheshimiwa Rais!
Napenda jambo hili lifahamike na lieleweke:
Ukweli ni kwamba jana, Disemba 19, 2013 sikuwepo Mwanza na wala sikutoka nje ya wilaya ya Kinondoni.
Ni imani yangu kuwa taarifa hii ilichapishwa makusudi. Ninaheshimu sana uhuru wa vyombo vya habari lakini kwa hili sasa mmezidisha.
Nakaribisha maoni yenu, kama taarifa kama hii isiyo sahihi na ya kupotosha ingechapishwa dhidi yako, ungechukua hatua gani?
Jumaa Kareem!
0 comments :
Post a Comment