-->

RAISI MURSI ALIEPINDULIWA MADARAKANI NA JESHI AONGEZEWA MASHTAKA YA KIJUBU


MAAFISA wa mashtaka wa Misri wanasema rais aliyeondolewa madarakani, Mohamed Morsi, atafikishwa mahakamani kwa makosa ya kutoroka jela wakati wa maandamano ya mwaka wa 2011 dhidi ya Rais Hosni Mubarak.

Watu wengine 132 watakabili mashtaka kama hayo, pamoja na kuwauwa walinzi wa gereza.

Washtakiwa wengine ni viongozi wa chama cha Bwana Morsi, cha Muslim Brotherhood, shekhe mmoja Yousef al-Qaradawi na wafuasi wa chama cha Wapalestina cha Hamas na cha Libnan, Hezbollah.

Bwana Morsi, rais wa kwanza wa Misri kuchaguliwa kwa misngi ya kidemokrasia, alitolewa madarakani na jeshi mwezi Julai.

Tayari Bwana Morsi anafanyiwa kesi kwa kuchochea mauaji ya wanaharakati wa upinzani wakati wa utawala wake wa mwaka mmoja.BBC

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment