THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Eng. Omari Jumanne Bakari kuwa Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO).
Kulingana
na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Desemba
04, mwaka huu, 2013. Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtafiti Mwandamizi katika Tume
ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam.
Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtanzania mwenye elimu, weledi
na uzoefu ambao umemfanya Mheshimiwa Rais aamini kuwa atakapoongoza SIDO,
atasaidia kukidhi matarajio ya taifa kwa kueneza ujasiriamali,
uwekezaji,uzalishaji na kutoa nafasi za ajira katika ngazi ya viwanda vidogo na
vya kati kama msingi imara wa uchumi wa Tanzania, ikiwemo kwa kuingiza sayansi,
teknolojia na ubunifu katika viwanda vidogo vidogo.
“Mwisho”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR
ES SALAAM.
16
Desemba, 2013
0 comments :
Post a Comment