Watu
wengi nimewasikia,wasomi na wasio wasomi wakijisifu kuwa wao wanaweza
kutawala, kuongoza n.k. Nami nimeona nisibaki nyuma kujisifu kuwa naweza
kutawala na kuongoza Taasisi inayohusu kada yangu. Watu hao wamekua
wakijisifu kwa kutopea sifa nyingi ambazo zingine hawana. Mfano; mi
nakubalika n.k. Lakini wanashindwa kufahamu kuwa kukubalika si wao
kujisifu ila kusifiwa. Ukiwatazama
wanakila sifa ya maovu hususan harufu ya Ufisadi na uroho wa madaraka
yaani"powermonger". Wanatumia nguvu nyingi kueeleza sifa zao huku
wakikataa mapungufu ili wajirekebishe. Pia,hata wanapozungumza hupenda
kueeleza mazuri tu bila mapungufu. Hupenda kulaum bila kutoa suluhisho.
Hujiona wajuzi wenye uwezo mkubwa wa akili na kudharau wachini yao.
Kipimo chao ni juhudi za kusifiwa hata kwa ujinga usio na maana. Sifa
zao ni nyingi ambazo mie nahisi kama nitakuwa nazo basi nahitaji
mnirekebishe kabla sijaanza uongozi na madaraka katika moja ya Kampuni
kubwa kulilko yote Tz yaani Ualimu. Wao huona wanaweza kwa kusifiwa na
kundi moja lenye sifa kama zao. Naomba wanaonijua basi mnieleze ukweli
wapi nakosea wapi napatia. Kiongozi mzuri ni yule anayetambua mchango wa
watu wengine aliowaacha kimapato, ujuzi hata maarifa. Kama ukishindwa
kuwathamini na kuwajali huwezi kuwa kiongozi mzuri hata kama utapewa
watu 03 uwatawale. Natamani sana kuwa kiongozi mwenye huruma, utu,
uzalendo wa wazi na uvumilivu. Hata hivyo sipendi majivuno, kujionesha
hata kujisifu ila nahitaji kusifiwa na kukosolewa pindi napo kwenda
kinyume. Napenda kipimo changu kisiwe kwa ndugu zangu tu bali hata kwa
wale wambali, majirani , rika za marafiki na wazee.
Unapoona unasifiwa harafu hufanikiwi ujue kuwa wanaokusifu ni wanafiki na wametopea kwenye kukula kisogo, hivyo yakupasa kufanya tathimini ya kina na ya kiutafiti ili kuweza kujilekebisha. Nimekuwa nikiwaona wanapotoa msaada hujitangaza na kujisifu, hili nalo linanihofisha. Kama nipo hivyo niambieni wala msiogepe, lengo ni kunifundisha niwe kama wale wenye kusifiwa na kuacha majivuno sifa na kiburi kwa watu wangu. Nafahamu kila mtu huwa na mapungu lakini mengine si ya asili bali ni tabia tu inayojengwa na mtu mwenyewe au jamii inauyomzunguka. Ukiona mtu wa kujifu kwa mafanikio tu mtilieni shaka sana, maana anakuwa na ufinyu wa fikra za kuwatumikia watu.
Mi nasema haya nipo kwenye mafunzo ili kesho nikilaumiwa muwe mmenilea vizuri nami nione uchungu wa kuwatumikia. Mwisho, naogopa sana kusifiwa kwa sifa ambazo sina. Hata kubadilika na kubagua watu kutokana na vipato vyao. Nishaurini niwe kama ......alivyo sifiwa kabla na baada ya kufa.
IMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA TWALIBU YASSINI MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU KATIKA CHUO KIKUU CHA KIISLAM MOROGORO

0 comments :
Post a Comment