Wakati
huo huo, Etoile hadi sasa haijailipa Simba SC fedha zake za kumnunua
mchezaji huyo na sakata lake limefikishwa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA).
Baada ya Okwi kukaa bila kucheza kwa miezi sita, Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) lilimpigania aruhusiwe kurejea nyumbani kuichezea SC Villa ya huko ili kunusuru kiwango chake.
Ukifuata historia hii unaweza kuona huyu ni mchezaji halali wa Etoile, inayodaiwa na Simba SC dola 300,000, lakini Yanga SC, wanasema wamejiridhisha wako sahihi kabisa katika kumsajili Okwi kutoka Villa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb alisema Jumapili mjini Dar es Salaam kwamba wamemsajili Okwi na ataanza kuichezea timu hiyo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na michuano ya Afrika kwa misimu miwili na nusu.
Bin Kleb alisema kwamba walimsajili Okwi tarkiban siku sita zilizopita, lakini Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ilipatikana Jumapili na ndiyo maana wakaamua kumtangaza siku hiyo.
“Tumefuatilia kote, hadi kwa wanasheria, na tumefanikiwa kupata hadi ITC yake, nawaambia mashabiki wa Yanga wajue viongozi wao wanafanya kazi, hatuna stori nyingi, sisi tunafanya vitendo, tunafanya kazi kwa siri sana,”. “Na tumepitia sehemu zote, tumeona kabisa tuko sahihi katika kumsajili mchezaji huyu na hakutakuwa na tatizo lolote upande wetu,”alisema.
Simba SC wamewajibu Yanga SC, wamewaambia wanajidanganya, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba watani wao wa jadi wameingia mkenge kumsajili Okwi na labda watamtumia kwenye mchezo wa Nani Mtani Jembe pekee, lakini zaidi ya hapo hatacheza Jangwani kwenye michuano yoyote rasmi.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba Okwi ni mchezaji halali wa Etoile du Sahel ya Tunisia na hawezi kucheza Yanga. “Mimi sina wasiwasi, naangalia tu sarakasi zao nikiwa najua wataangukia wapi. Yule mchezaji Yanga wameingizwa mkenge na FUFA (Shirikisho la Soka Uganda). Kwa sababu, Etoile ilimtoa kwa mkopo SC Villa na ndiyo maana hata FUFA walipotaka kumtumia katika CHAN, wakaambiwa haiwezekani kwa kuwa yule ni mchezaji wa Etoile,”alisema Hans Poppe.
Kwa undani zaidi, Yanga wanasema walikwenda hadi FIFA wakapewa hati ya hukumu ya kesi ya Okwi na Etoile. Wanadai Okwi alifungua mashitaka FIFA dhidi ya Etoile kupitia wakili wake, akilalamika kukiukwa kwa vipengele vya Mkataba baina yake na klabu hiyo ya Tunisia na akafanikiwa kushinda kesi hiyo kwa FIFA kuuvunja Mkataba baina ya pande hizo. Hao Yanga wanasema.
Lakini Simba SC nao, wanasema Okwi alipokwenda Tunisia baada ya muda mfupi akapewa ruhusa ya kurejea Uganda kuchezea timu ya taifa, lakini akachelewa kurejea Tunis.
Alipokwenda baadaye, akaadhibiwa kwa kukatwa mshahara wa kipindi chote ambacho hakuwepo kazini, pamoja na kuteremshwa hadi kikosi cha pili. Simba wanasema Okwi akasusa kujiunga na kikosi cha pili, akawa anakaa tu bila kufanya mazoezi hadi alipoamua kurejea Uganda.
Wanasema baada ya Okwi kushindwa kuelewana na Etoile, FUFA ikamuombea uhamisho wa mkopo na klabu ya Tunisia ikakubali kumpa miezi sita kurejea kuchezea SC Villa. Hao Simba wanasema.
Imekuwa vigumu kupata mapema maelezo ya Etoile juu ya sakata hilo, lakini kwa kuwa Yanga imemsajili Okwi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lina utaratibu mzuri tu wa kufuata kabla ya kumuidhinisha mchezaji kuichezea klabu, basi ufumbuzi wa suala la Okwi utapatikana muda si mrefu.
Tayari hii ni kesi, huu si usajili mwepesi, wazi Yanga watatakiwa kutoa vielelezo zaidi vya uhalali wa kumsajili Okwi ikiwemo hiyo barua wanayodai wanayo ya hukumu ya mchezaji huyo kutoka FIFA. TFF itawasiliana na kitengo husika cha FIFA kilichoendesha kesi hiyo na ikithibitisha ni kweli Mganda huyo alishinda kesi, basi ataichezea Yanga SC.
Yote kwa yote, bado haifuti deni la Etoile kwa Simba SC la dola za Kimarekani 300,000 kama kweli yalikuwapo makubaliano ya kiwango hicho cha fedha kwa ajili ya mauziano ya mchezaji huyo, basi zitalipwa.
Na kwa sababu kuna kanuni ya FIFA inayosema klabu inatakiwa kuwa imemaliza kulipa malipo ya fedha za kumnunua mchezaji kabla ya kumaliza Mkataba wake au kumtoa sehemu nyingine, sasa Etoile watalazimika kuilipa Simba SC mara moja kama walishindwa kesi na Okwi.
Simba SC wangekuwa wamekwishafika katika hatua nzuri kwenye madai hayo, kama wangekuwa wamelipa ada ya dola za Kimarekani 10,000 baada ya kufungua kesi FIFA, lakini kwa kupeleka malalamiko bila ada hiyo, kesi yao haijawezwa kusikilizwa. Ila sasa ili kupata haki yao, Simba lazima walipe fedha hizo FIFA iweze kuisikiliza kesi hiyo na kutoa hukumu.
Kama kweli Simba waliandikishiana na Etoile malipo yanayotajwa, basi wana Simba hawana haja ya kuwa na kimuhemuhe, fedha zao zitalipwa tu. Ila hili, la Okwi kusaini Yanga, ni kesi nyepesi sana kwa TFF na wala haitawatoa jasho.
Yanga watatakiwa kuwasilisha vielelezo na TFF watawasiliana na FIFA kupata ukweli wa sakata la mchezaji huyo na baada ya hapo, watamuidhinisha au kutomuidhinisha, kulingana na majibu watakayoyapata kutoka bodi hiyo ya soka duniani. Jumatano njema.
chanzo:bin zubery

0 comments :
Post a Comment