Taarifa ya mkutano wa
wanachama wa chama cha mapinduzi wa maeneo ya District of Colombia, Maryland na
Virginia ( DMV)
Tunaombwa kwa umoja wetu kuhudhuria mkutano wa
wanachama wote ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu kuimarisha tawi letu.Pia
fomu za kugombea nafasi ya wajumbe 10 wa halmashauri kuu ya tawi, katibu UWT,
katibu Wazazi na Mwenyekiti umoja wa vijana zinapatikana, tafadhali wasiliana
na viongozi ili upewe maramoja ujaze na kuziwakilisha kabla ya mkutano.
Tunawakaribisha wote wanaotaka kujiunga
na CCM uandikishwaji wa wanachama wapya utakuwepo siku ya mkutano.
Tafadhali usikose
kuhudhuria ili sauti yako isikike na ushiriki kikamilifu kukijenga chama chetu
na kuleta maendeleo ya nchi yetu.
MAHALI:
1400 University Boulevard Langley Park,
Maryland 20783 (
TABEER RESTAURANT)
SIKU: Jumapili, DECEMBER 15, 2013
SAA: 5.00 p.m -8 pm
1. Taarifa fupi ya Tawi
2. Mikakati juu ya uimarishaji wa tawi letu
3. Uchaguzi wa viongozi wa tawi( NAFASI ZILIZOWAZI)
4. Mengineyo
Tafadhali tujitokeze kwa wingi kama ilivyo desturi yetu kina Baba
tunaomba maji na soda na kina Mama Vitafunio. Tafadhali zingatia muda.
Asanteni
Uongozi wa CCM Tawi la DMV
0 comments :
Post a Comment