Dar es
Salaam. Wakati Bunge la Kujadili Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania linaanza kikao chake kesho mjini Dodoma, wasomi na
wanazuoni wapatao 300 wanakutana Dar es Salaam leo kujadili rasimu hiyo,
mjadala mkuu ukilenga Muundo wa Serikali unaofaa nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Umoja wa Utafiti wa Programu za Vyuo Vikuu Kusini
na Mashariki mwa Afrika (ESAURP), Profesa Teddy Malyamkono alisema Dar
es Salaam jana kwamba kongamano hilo litajadili tafiti za wasomi hao
ambazo zimekusanywa katika kitabu kimoja.
Alisema
kitabu hicho ambacho kinajulikana kama Katiba Bora Tanzania,
kinajumuisha mada mbalimbali ambazo zinalenga kuibua mjadala juu ya nani
atakayenufaika na Muungano wa Serikali Tatu kama mapendekezo ya Rasimu
itakayojadiliwa bungeni yanavyoeleza.
Pia
kongamano hilo litajadili na kuchambua gharama za Serikali hizo na hasa
maswali kama zitabebwa na nani? Zitasimamiwa na nani? Na vipi Zanzibar
ambayo asilimia 90 ya wakazi wake ni Waislamu itamudu kujiepusha na
masuala ya udini.
"Tunataka
Muungano ambao utaendeleza mshikamano uliopo ndani ya nchi hivi sasa,"
alisema na kuongeza kuwa kuna vitu vingine vya kujadili iwapo Muungano
utakuwa wa Serikali Tatu.... "Kama zitakuwa Serikali Tatu, nini hatima
ya nchi hizo zilizoungana hususan katika uhusiano na mataifa mengine
ambayo hayana ushirikiano na upande mmoja?"
Awali,
akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Shule ya Sheria katika Chuo
Kikuu Dar es Salam (UDSM), Profesa Boniventure Rutinwa alisema kuna mada
ambayo itaakisi mapendekezo ya Kundi la G55 ambalo lilipendekeza mfumo
wa Serikali Tatu lakini likapingwa bungeni. Profesa Boniventura pia
aliikosoa Tume ya Warioba iliyokuwa ikikusanya maoni kuwa ilikuwa na
walakini kwa kutokuwa na hadidu za rejea kama tume nyingine ikiwamo ile
ya Jaji Robert Kisanga ambayo nayo pia ilikuwa na mapendekezo ya muundo
wa Serikali Tatu.Dar es Salaam. Wakati Bunge la Kujadili Rasimu ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaanza kikao chake kesho
mjini Dodoma, wasomi na wanazuoni wapatao 300 wanakutana Dar es Salaam
leo kujadili rasimu hiyo, mjadala mkuu ukilenga Muundo wa Serikali
unaofaa nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Umoja wa Utafiti wa Programu za Vyuo Vikuu
Kusini na Mashariki mwa Afrika (ESAURP), Profesa Teddy Malyamkono
alisema Dar es Salaam jana kwamba kongamano hilo litajadili tafiti za
wasomi hao ambazo zimekusanywa katika kitabu kimoja.
Alisema
kitabu hicho ambacho kinajulikana kama Katiba Bora Tanzania,
kinajumuisha mada mbalimbali ambazo zinalenga kuibua mjadala juu ya nani
atakayenufaika na Muungano wa Serikali Tatu kama mapendekezo ya Rasimu
itakayojadiliwa bungeni yanavyoeleza.
Pia
kongamano hilo litajadili na kuchambua gharama za Serikali hizo na hasa
maswali kama zitabebwa na nani? Zitasimamiwa na nani? Na vipi Zanzibar
ambayo asilimia 90 ya wakazi wake ni Waislamu itamudu kujiepusha na
masuala ya udini.
"Tunataka
Muungano ambao utaendeleza mshikamano uliopo ndani ya nchi hivi sasa,"
alisema na kuongeza kuwa kuna vitu vingine vya kujadili iwapo Muungano
utakuwa wa Serikali Tatu.... "Kama zitakuwa Serikali Tatu, nini hatima
ya nchi hizo zilizoungana hususan katika uhusiano na mataifa mengine
ambayo hayana ushirikiano na upande mmoja?"
Awali,
akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Shule ya Sheria katika Chuo
Kikuu Dar es Salam (UDSM), Profesa Boniventure Rutinwa alisema kuna mada
ambayo itaakisi mapendekezo ya Kundi la G55 ambalo lilipendekeza mfumo
wa Serikali Tatu lakini likapingwa bungeni. Profesa Boniventura pia
aliikosoa Tume ya Warioba iliyokuwa ikikusanya maoni kuwa ilikuwa na
walakini kwa kutokuwa na hadidu za rejea kama tume nyingine ikiwamo ile
ya Jaji Robert Kisanga ambayo nayo pia ilikuwa na mapendekezo ya muundo
wa Serikali Tatu.
CHANZO:MWANANCHI
0 comments :
Post a Comment