Mshambuliaji wa klabu ya
Manchester United Wayne Rooney jana usiku hatimaye alimaliza tetesi za
kuhusu hatma yake ndani ya klabu hiyo baada ya kusaini mkataba mpya
utakaomuweka kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2019. Rooney ambaye
alisajiliwa na United akitokea Everton mwaka 2004, amesaini mkataba mpya
wa miaka minne wenye thamani ya £300,000 kwa wiki. Rooney sasa analipwa jumla ya £15.6m kwa mwaka - kwa maana
MGAWANYIKO WA MSHAHARA MPYA WA ROONEY
£15,600,000 kwa mwaka
£300,000 wiki
£43,000 kwa siku
£1,800 kwa saa
£30 kwa dakika
50p kwa sekunde
hiyo Rooney sasa
amemfunika Cristiano Ronaldo aliyekuwa akishika nafasi ya kwanza kwa
kulipwa fedha nyingi za mshahara - Ronaldo mkataba wake mpya na Real
Madrid analipwa kiasi cha £288,000 kwa wiki. Pia amemfunika Leo Messi
ambaye analipwa kiasi cha £12.08m kwa mwaka, hii ni kwa mujibu wa 2013 Forbes rich list.
0 comments :
Post a Comment