IKIWA
imebaki siku moja kabla ya Galatasaray kuikaribisha Chelsea katika
mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, kumezuka vurugu za kupigana na
kurushiana viti kati ya mashabiki wa Galatasaray na mahasimu wao
Besiktas katika mitaa ya jiji la Istanbul. Kumekuwa na picha za video
katika mtandao wa Youtube ukionyesha makundi makubwa ya wahuni wa
Galatasaray na Besiktas wakichapana katika mitaa yenye maduka mengi
kabla ya mchezo baina ya timu hizo katika Uwanja wa Turk Telekom.
Vurugu
hizo ziliendelea pia wakati wa mchezo huo ambao Galatasaray ilishinda
kwa bao 1-0. Mashabiki wa Chelsea watakaosafiri kwenda jijini Istanbul
kwa ajili ya kuishangilia timu yao wameonywa kuwa makini pindi
watakapokuwa huko. (EL)
0 comments :
Post a Comment