Watu 21
wameuwawa hadi kufikia jana Alhamisi katika mapambano mapya kati ya
polisi wa kutuliza fujo na waandamanaji mjini Kiev,Ukraine wakati
mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wakikutana na Rais Vikctor
Yanukovich.
Mapambano
mapya yameibuka kati ya polisi wa kutuliza fujo na waandamanaji leo hii
katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev, na kutibua mpango tete wa suluhu
wakati mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wakikutana na Rais
Vikctor Yanukovich kujaribu kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo.
Mapambano
hayo ya jana yalizuka wakati waandamanaji waliojifunukia nyuso
walipowarushia polisi wa kutuliza fujo mabomu ya petroli na mawe katika
uwanja wa Uhuru mjini Kiev ambacho ni kitovu cha mzozo wa kisiasa wa
jimbo hilo la zamani la Muungano wa Kisovieti.
Waanadamanaji
hao walifanikiwa kuwarudisha nyuma polisi kwa kama mita 200 na na
kuweza kuudhubiti tena uwanja huo wote ambao waanadamanaji wanaopinga
serikali walikuwa wakiukalia kwa mabavu tokea mwezi wa Novemba mwaka
jana.
Polisi
ilitumia risasi za mpira kujaribu kuzima shambulio la waandamanaji hao
na imedai kwamba mashambuliaji wa kuvizia amewajeruhi polisi 20 kwa
kuwafyetulia risasi za moto kutoka kwenye jengo linaloelekezana na
uwanja huo ulipgubikwa na moshi.
Polisi
ilitumia risasi za mpira kujaribu kuzima shambulio la waandamanaji hao
na imedai kwamba mashambuliaji wa kuvizia amewajeruhi polisi 20 kwa
kuwafyetulia risasi za moto kutoka kwenye jengo linaloelekezana na
uwanja huo ulipgubikwa na moshi.
Mapambano
hayo yametibua suluhu waliokubaliana kati ya Rais Viktor Yanukovych na
viongozi wa upinzani masaa machache kabla kufuatia umwagaji damu
uliogharimu maisha ya takriban watu 28 katika kipindi cha siku mbili.
Taarifa
fupi iliyochapishwa kwenye wovuti wa ofisi ya rais hapo jana usiku
haikutowa maelezo suluhu hiyo inamaanisha nini au itatekelezwa vipi na
wala haikufafanuwa mazungumzo yatafanyika vipi na pia haikodokeza iwapo
yatakuwa tafauti na mikutano iliofanyika huko nyuma kati ya rais na
viongozi wa upinzani.
Mbinu za
kisiasa na za kidiploamasia zimekuwa zikiendelezwa ambapo pande zote
mbili Urusi na mataifa ya magharibi zimekuwa mbioni kujenga ushawishi
wao kwa nchi hiyo. Mawaziri watatu wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya
kutoka Ujerumani,Ufaransa na Poland wako Kiev leo hii kuzungumza na
pande mbili zinazohasimiana kabla ya mkutano wao wa dharura wa Umoja wa
Ulaya mjini Brussels ili kufikiria hatua za kuchukuwa dhidi ya wale
waliohusika na umwagaji damu wa hivi karibuni nchini humo.
Waziri wa
mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amezungumza na waziri mwenzake wa
Ujerumani Frank -Walter Steinmeier na kumtaka kutumia mawasiliano yake
ya karibu na ya kila siku na upinzani wa Ukraine kutafuta ufumbuzi wa
mzozo huo.
Wizara ya
mambo ya nje ya Urusi imeelezea ghasia hizo kuwa ni jaraibio la
mapinduzi na hata kutumia neno "mapinduzi ya kibaguzi" kwa kuyafananisha
na kusimama kwa utawala wa Manazi nchini Ujerumani hapo mwaka 1933.
Wizara hiyo imesema Urusi itatumia ushawishi wake wote kurudisha amani
na utulivu nchini humo.
Rais
Barack Obama wa Marekani pia amelaani umwagaji damu uliotokea na kuonya
kwamba itaichukulia hatua nchi hiyo iwapo hali hiyo itaendelea ikiwa ni
pamoja na uwezekano wa kujiuga na Umoja wa Ulaya kuiwekea vikwazo
Ukraine.
Askari wa Ukraine wakiwadhibiti wananchi
Raia wa Ukraine akirusha chupa yenye mafuta kwa askari wa kutuliza ghasia
Baadhi yawananchi wa Ukraine wakisali kutokana na machafuko nchini humo
Wananchi waliofariki wakiwa wamefunikwa kwa bendera ya nchi hiyo na pia wakiwa wamewekewa maua kwenye miili hiyo
Mapigano yakiendelea
shukrani pamoja pure blog
0 comments :
Post a Comment