-->

SERIKALI YA RAISI MUGABE YAWAACH HURU TAKRIBAN WAFUNGWA 2000

Headlines News :

Serikali ya Zimbabwe imetangaza kuwa imewaachia huru karibu wafungwa 2,000 waliokuwa wakishikiliwa gerezani kutokana na makosa mbalimbali.
Taarifa kutoka Harare zinasema kuwa, wafungwa wote wanawake wameachiliwa huru isipokuwa wale wanaotumikia adhabu ya vifungo vya maisha na waliohukumiwa adhabu ya kifo. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wafungwa wote walio na umri chini ya miaka 18 wameachiwa huru, bila kuzingatia makosa waliyofanya. Taarifa ya serikali ya Zimbabwe imeeleza kuwa, msamaha huo pia umewajumuisha  wafungwa wagonjwa, wafungwa wenye umri wa zaidi ya miaka 70 na wale waliohukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu na chini ya hapo na  hadi sasa tayari wameshatumikia robo ya adhabu zao.
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu lilitangaza kwamba, mamia ya wafungwa walifariki dunia wakati Zimbabwe ilipokuwa ikikabiliwa na makali ya vikwazo vya nchi za Magharibi mwaka 2008.
Katiba mpya ya Zimbabwe iliyotiwa saini mwaka 2013, ilitengua adhabu ya kifo kwa wanawake, watu wenye umri wa chini ya miaka 21 wakati wa kutenda jinai na watu wenye umri wa zaidi ya miaka 70.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment