-->

CHADEMA WATOA SIKU TATU KWA MH RAISI KIKWETE KUWEZA KUIFUTA KAULI YAKE



CHADEMA WATOA SIKU TATU KWA RAIS KIKWETE KUFUTA KAULI

Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kufuta kauli yake ya kuwataka wana CCM kuacha unyonge na kujibu mapigo dhidi ya upinzani na ametakiwa kuomba radhi ndani ya siku tatu, vinginevyo suala hilo litafikishwa jumuiya za kimataifa.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kufunga Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo Chadema wanaitafsiri kama kielelezo cha kuvuruga amani ndani ya nchi.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa CHADEMA, Benson Kigaila alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kufuta alichokizungumza ndani ya siku tatu kuanzia jana, vinginevyo watalifikisha suala hilo mbele ya jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya malalamiko yao.

Alisema kuwa Rais Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu, na alihoji kwanini awatake Wana-CCM kujibu mapigo dhidi ya wapinzani badala ya kuacha hatua za kisheria zikafuatwa kwa kutumia vyombo husika ambavyo ni polisi na majeshi na mahakama.

Alipotafuta Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, ili kuelezea tishio la CHADEMA, alisema alisema “Kauli aliyoitoa Rais Kikwete ni ndogo na imetokana na vitendo vinavyofanywa na viongozi na wanachama wa CHADEMA kuvuruga amani nchini.”
CHANZO:DAR 24
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment