Mwenyekiti
wa TCD, James Mbatia alitangaza maazimio hayo juzi wakati wakufunga
mkutano wa siku mbili uliohusu tafakuri na maridhiano kuelekea Bunge
maalum la Katiba.
Dar es
Salaam.Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kimetoa maazimio 16 likiwemo
la wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kujenga hoja na kuepuka kusukumwa
na maslahi binafsi na ya vyama vyao vya siasa katika mchakato wa kupata
Katiba mpya.
Mwenyekiti
wa TCD, James Mbatia alitangaza maazimio hayo juzi wakati wakufunga
mkutano wa siku mbili uliohusu tafakuri na maridhiano kuelekea Bunge
maalum la Katiba.
" Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba tuepuke kusukumwa na misimamo binafsi, ya
vyama na ya makundi tunayoyawakilisha," alisema Mbatia akitoa maazimio
hayo.
Mbatia
alisema wameazimia kuwa kuna umuhimu wa kuchagua viongozi wa Bunge
Maalum kwa kuzingatia uadilifu, weledi, uzalendo na uzoefu ili waweze
kutetea maslahi ya taifa.
Azimio
jingine lililotolewa kwenye mkutano huo ni Bunge Maalum kuzingatia
rasimu ya Katiba, taarifa ya Tume ya Katiba na maoni yanayoendelea
kutolewa na makundi mbalimbali katika jamii.
Mbatia alisema pia kuwepo kwa mfumo wa utekelezaji wa haki za binadamu pamoja na haki za makundi maalum yaliyopo katika taifa.
" Pia
kuwepo kwa muundo wa dola unaozingatia mgawanyo bora wa madaraka baina
ya Serikali, Bunge na Mahakama ili vyombo hivyo viweze kutimiza majukumu
yake kwa ufanisi, uwazi bila kuingiliana," alisema Mbatia.
Azimio
jingine ni kwa TCD kuendelea kuandaa na kuratibu mijadala ya kujenga
maridhiano katika kipindi chote cha mchakato wa Katiba.
CHANZO:MWANANCHI
0 comments :
Post a Comment