Raia
wa Henellic, Alexamdrios Atanasios, amekamatwa maafisa wa usalama wa
Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumapili usiku
Februari 24, 2014, akiwa na kilo tano za madawa ya kulevya.
Kwa
mujibu wa duru za kiusalama uwanjani hapo, raia huyo alikamatwa wakati
wa upekuzi, akijiandaa kupanda ndege ya Swiss air akielekea mjini
Zurich.
Kwa
mujibu w aduru hizo za usalama, madawa hayo yalikutwa yakiwa yamefichwa
kwenye “sakafu” ya begi lake baada ya mitambo ya kisasasa ya upekuzi,
kugundua kuwa kulikuwa na ‘mzigo’.
Habari
zinasema, kwa sasa mtuhumiwa anashikiliwa kwenye kituo cha polisi cha
uwanja wa ndege akisubiri taratibu za kisheria ili afungukliwe mashtaka
chanzo:matukio na vijana
0 comments :
Post a Comment