Serikali ya Burundi imezindua mradi wa dola milioni 25 za Kimarekani kwa ajili ya mtandano wa Intaneti wenye kasi kubwa nchini humo.
Mradi huo umezinduliwa leo huko Bujumbura na Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo ambaye amesema mashirika manne binafsi na serikali ndio wamiliki wa mkongo wa taifa wa mawasiliano (fiber optic) wenye lengo la kuhakikisha wananchi wote wanapata Intaneti kwa bei nafuu ifikapo mwaka 2025. Tayari kebo ya mkongo huo wenye urefu wa kilomita 1,000 imeshawekwa katika mikoa 17 ya nchi hiyo. Kebo hiyo itaunganishwa na kebo za chini ya bahari ambazo zinaunganisha Afrika na dunia nzima kupitia bandari za Mombasa, Kenya, na Dar-es-Salaam Tanzania. (R.M).
Benki ya Dunia imefanya utafiti unaoonyesha kuwa kuimarika kwa asilimia 10 kasi Intaneti kunaweza kuongeza pointi asilimia 1.4 katika ustawi wa kiuchumi kila mwaka. Burundi ina idadi ya watu milioni 8 na kasi yake ya Intaneti iko chini sana ikilinagnishwa na nchi nyingine za eneo la mashariki mwa Afrika.
Chanzo, kiswahili.ibir.ir/habari
0 comments :
Post a Comment