-->

CCM WAFUNGUA RASMI KAMPENI ZA KUWANIA KITI CHA UBUNGE KALENGA KUPITIA GODFREY MGIMWA

mgimwajr 40707
Mgombea wa ubunge jimbo la kalenga kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Godfrey Mgimwa amewataka wananchi wa jimbo hilo kumpa kura kwa sababu ni yeye pekee kupitia chama chake atayaendeleza yaliyoachwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo Dk. William Mgimwa.
Mgimwa ambae pia ni mmoja wa watoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa fedha, Dk. Mgimwa aliyasema hayo juzi wakati wa kampeni ilyofanyika katika kata ya Mseke.

Anasema kuwa kati ya vitu atakavyovifanya endapo atachaguliwa na wanakalenga ni kumalizia yale yalioanza kufanywa na baba yake na kuwa malengo yake ni pamoja na kushughulikia barabara itokayo Njia panda ya tosa kuelekea hospitali teule ya Ipamba, kuboresha huduma za afya hususani zahanati za kila kijiji kama sera ya chama hicho inavyoagiza na elimu ya msingi na sekondari.

Anasema wananchi wanatakiwa kumchagua mbunge anaetambua kuwa nini kinachofanyika kalenga na kipi kinatakiwa kufanyika ili kuleta maendeleo ndani ya jimbo hilo.

"Wananchi na wapiga kura wa jimbo la kalenga mnatakiwa kumchagua mbunge anaejua nini matatizo yakalenga na ni yapi yamefanyika na ambayo bado hayajafanyiwa kazi ili nikayafanyie kazi mpaka kuhakikisha changamoto tunazipunguza ikiwezekana kumaliza kabisa"alisema Godfrey

Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu anasema ni vema wanakalenga wakamchagua kijana ambaye atatumia muda wake mwingi katika kujishughulisha na maendeleo ya jimbo hilo.

Anasema hakuna ubaya wowote kwa mtoto wa kiongozi kuwania nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na mzazi wake na kuwa ni CCM pekee inayoweza kuwatatulia kero zao kwa kuwa ilianza kuzishughulikia tangu mbunge aliyepita.

Uchaguzi wa Jimbo la Kalenga utafanyika Machi 16 mwaka huu baada ya kifo cha Mbunge wa jimbo hilo Dk. Mgimwa ambaye alikuwa Waziri wa Fedha mwishoni mwa mwezi wa 12 mwaka jana. Chanzo: Hakimu Mwafongo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment