Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Rukia Fungameza[20]mkazi
wa mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya
kwa tuhuma za kutupa chooni kichanga jinsi ya kiume na kusababisha kifo chake.
Mwenyekiti wa mtaa huo Juma Mbuza amesema walimtilia shaka
mtuhumiwa Februari 18 mwaka huu katika kilabu cha pombe za kienyeji baada ya
kutoonekana na ujauzito,ndipo walipomuulza kulikoni naye kudai kuwa amejifungua
lakini mtoto yupo nyumbani.
Kauli hiyo haikumridhisha Mwenyekiti huyo ndipo alipoamua
kumtafuta balozi wake aitwae Daud Dule na kumuuliza mtoto yupo wapi ndipo
alipoanza kuwa na wasiwasi hali iliyowalazimu kumkamata kutoa taarifa kituo cha
Polisi Iyunga ambapo kabla ya kufika Kituoni majira ya saa kumi na moja jioni
mtuhumiwa alikiri kujifungua na kutupa kichanga chooni Februari 18 mwaka huu.
Baada ya taarifa hiyo mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa kituo
kikuu cha kati Febuari 19 ambapo Polisi hawakuweza kufika eneo la tukio licha
ya Mwenyekiti wa mtaa kufuatilia mara kwa mara kwa mkuu wa kituo cha Polisi
Iyunga ambapo alijibiwa kuwa watafika.
Hata hivyo baada ya Polisi kutofika eneo la tukio kwa siku mbili
tangu kukamatwa mtuhumiwa Mwenyekiti wa mtaa alitoa taarifa katika kikao cha
kata Februari 21 kufuatia tukio lililotukia mtaani kwake na Polisi
kushindwa kufika kwenye tukio siku tatu baada ya tukio hali ambayo ilikuwa kero
mtaani kwake.
Polisi walifika eneo la tukio Februari 22 majira ya saa tano na
nsu asubuhi wakiambatana na Kikosi cha Zimamoto Jiji la Mbeya ndipo walipoanza
anza kuibua mwili wa mtoto ambapo ulikutwa umeharibika vibaya kutokana na kukaa
kwa muda wa siku nne bila kuibuliwa umbali wa kilometa saba tu kutoka Jijini.
Baada ya mahojiano mtuhumiwa alidai sababu za kutupa kichanga
hicho cha kiume ni kutokana na kuogopa aibu kwa mumewe aliyepo Songea mkoani
Ruvuma kikazi ambapo mimba hiyo aliipata nje ya ndoa.
Uchunguzi umebaini kuwa mwanamke huyo aliagizwa na mumewe kurejea
Songea mwishoni mwa mwaka jana lakini alikataa akidai kuwa angeenda mwaka huu
baada ya kumsaidia kaka yake shughuli za palizi.
Kabla ya kichanga kilichotupwa chooni mtuhumiwa ana mtoto mwingine
jinsi ya kike anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili na nusu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa amelilalamikia Jeshi la Polisi
kwa kutoenda eneo la tukio mapema hali ambayo inasababisha wananchi
kujichukulia sheria mkononi hali ambayo inweza kuepukika.
Baadhi ya mashuhuda akiwemo mama Emilly Amnoni na Paulo Mbawala
wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo kwani wamedai ni cha
kinyama na ni cha kwanza mtaani kwao hivyo wanaomba sheria iweze kuchukua
mkondo wake ili kukomesha kabisa vitendo vya kikatili Mkoani Mbeya.
Rukia Fungameza[20]mkazi wa mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi Anaetuhumiwa kutupa mtoto chooni |
Mashuhuda wakishudia tukio lenyewe |
Mashuhuda wakishudia tukio lenyewe |
Akina mama wakiwa na uchungu wengine wakilia kutokana na tukio hili la kinyama |
Hili ndili shimo ambalo mtuhumiwa huyu alikili kumtupa mtoto huyo hapa |
Mwenyekiti
wa mtaa huo Juma Mbuza mwenye Flana ya bluu akiwa na barozi kushoto na
mashuhuda wengine wakimsikiliza mwenyekiti huyo. CHANZO:SHADDY CLASSIC |
Hapa usafi ukifanyika baada ya oparesheni ya kutafuta mwili wa mtoto alietupwa |
0 comments :
Post a Comment