-->

JULIUS MTATILO MTETEZI WA WANYONGE KUONGOZA HARAKATI ZA KUPINGA MADAI YA ONGEZEKO LA POSHO


  Naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF MH: Julius Mtatilo, ataongoza kupinga ongezzeko la Posho wanazodai wabunge wa Bunge maalum la mabadiliko ya Katiaba.
  Akiandika katika ukurasa wake wa Facebook Mtatilo ambaye naye pia ni Mbunge wa Bunge ilo amesema atahakikisha anakusanya sahihi za wajumbe wa bunge la katiba wanaopinga ongezeko ilo.
Julius S. MtatiroMAPAMBANO YA KUZUIA ONGEZEKO LA POSHO JUU YA MAISHA YA WANANCHI MASIKINI YANAENDELEA;
Jumatatu asubuhi nitaanzisha zoezi la kukusanya sahihi za wajumbe wa bunge la katiba wanaopinga ONGEZEKO LA POSHO.

Kazi hiyo nitaifanya kila muda wa mapumziko, ifikapo jumatano tutaunganisha sahihi zote na kumuandikia Rais wa JMT barua rasmi na hoja za kupinga posho hizo.

Kwa mujibu wa kifungu cha 29(2) cha sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 (toleo la mwaka 2014), Rais Kikwete anayo mamlaka ya kuzuia njama zozote za kuongeza posho.

Jambo hili lazima tulifanye kwa maneno na kwa vitendo, lina RISKS zake, tutashutumiwa, tutakejeliwa, tutapigwa vita, tutapewa majina ya kutafuta umaarufu n.k.

Matusi yote hayo ni bora mara mia moja kuliko kujaza matumbo yetu huku mshahara wa mwalimu kwa mwezi ni shs laki tatu (300,000/-)
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment