-->

NCHI ZA MAGHARIBI ZAENDELEA KUONDOA MISAADAA YAO BAADA UYA UGANDA KUUNDA SHERIA YA KUZUIA USHOGA NA USAGAJI

Wamagharibi waikatia Uganda misaada ya fedhaSiku chache baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kusaini muswada wa sheria ya kupinga liwati na usagaji katika nchi yake, nchi kadhaa za Magharibi zimetangaza kuikatia misaada serikali ya Kampala kufuatia hatua hiyo. Serikali ya Uholanzi imetangaza leo kwamba itaondoa misaada yake ya takriban dola milioni 8 kwa serikali ya Uganda na kwamba misaada hiyo sasa itapewa makundi ya kiraia. Norway na Denmark pia zimetangaza kwamba zitapunguza misaada yake kwa Uganda baada ya Rais Museveni kuidhinisha sheria inayopiga marufuku liwati na usagaji. Katika radiamali yake kwa hatua hiyo, serikali ya Kampala imesisitiza kwamba, haitalegeza kamba katika kulinda utamaduni wa wananchi wake na ule wa bara la Afrika kwa ujumla. Msemaji wa serikali ya Uganda, Ofwono Opondo amesema Wamagharibi wanaweza kuondoa misaada yao lakini Kampala haitabadili msimamo wala kufuta sheria hiyo. Rais Museveni kwa upande wake amelaani hatua ya Wamagharibi ya kuikatia misaada nchi yake akisema Uganda si jaa la takataka la kuhifadhi uchafu wote wa wakoloni mamboleo
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment