-->

MSEVENI AKERWA NA RAISI OBAMA KUINGIALIA MAMBO YA NDANI KATIKA NCHI YAKE,ATISHIA KUJIUNGA NA URUSI

Raisi Yoweri Museveni.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametoa matamshi makali dhidi ya Rais Barack Obama wa Marekani akimtaka akome kungilia masuala ya ndani ya Uganda.
Matamshi hayo makali yamekuja baada ya Rais wa Marekani kutishia kuwa uhusiano wa nchi yake na Uganda utaharibika iwapo Rais Museveni atasaini na kuufanya kuwa sheria muswada wa kupinga vitendo vichafu vya kujamiiana watu wa jinsia moja.
   Agusia Kushirikiana na Russia.
Rais Museveni amesema, atashirikiana na Russia iwapo Marekani itaendelea kuingilia masuala ya ndani ya Uganda na kuongeza kama ninavyomnukuu:
“Russia imekuwa ikifanya shughuli zake barani Afrika tangu mwaka 1917 yaani kwa zaidi ya miaka 100. Ninataka kushirikiana na Russia kwa sababu hawachanganyi siasa zao na siasa za nchi nyingine.” Mwisho wa kunukuu
CHANZO:MATUKIO NA VIJANA
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment