Sheikh Abdul Alim Musa Imam wa Masjid al Islam mjini Washington Marekani amesema kuwa, shambulio la Septemba 11, 2001 lilipangwa na kutekelezwa na Wamarekani wenyewe kwa lengo la kutangaza vita dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu na Waislamu duniani.
Sheikh Abdul Alim Musa amekosoa vikali maamuzi ya jaji wa mahakama moja nchini Marekani aliyekataa kufungua mashtaka ya ujasusi uliofanywa na polisi ya New York dhidi ya madrasa za kidini, misikiti na Waislamu wa New Jersey na kuongeza kuwa, serikali inafanya mambo kinyume cha sheria nchini humo.
Imam wa Masjid al Islam mjini Washington ameiambia kanali ya televisheni ya al Alam kwamba na hapa tunamnukuu: 'Mtazamo wangu ni huu kwamba, ni bure kwa Waislamu kutumia nguvu zao kwa lengo la kupigania uadilifu nchini Marekani. Mfumo wa kisheria na kimahakama nchini humo unadhibitiwa kikamilifu na Wazayuni na kwamba Waislamu hawatakuwa na fursa ya kuamiliwa kwa usawa katika mfumo wa kimahakama na kisheria nchini humo', mwisho wa kunukuu. Sheikh Abdul Alim Musa ameongeza kuwa, Waislamu wa Marekani na ulimwenguni kote wamechoshwa na vitendo vya kijasusi vinavyofanywa na nchi hiyo.
Chanzo, kiswahili.irib.ir
R.M
0 comments :
Post a Comment