MSAFARA wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo ulishindwa kupita katika msitu wa Sao Hill Mufindi Iringa,Rais Kikwte alishindwa kupita eneo hilo baada ya Barabara Kuu ya Iringa -Mbeya kuzibwa na moshi mkubwa uliotokana na moto huo, Rais alikutana na hali ikiwa ni saa takribani mbili tangu alipofunga kikao chake cha majumuisho ya ziara yake Mkoani humo na viongozi wa Mkoa wa Njombe na kuwataka kuchukua hatua katika kuthibiti majanga ya moto ili kuepusha ukame
Moto uhuo ulioanza kuwaka saa nane mchana ulikwamisha msafara huo wa Rais Kikwete katika eneo la Changalawe mjini Mafinga umbali wa mita 2 kufika njia panda ya kuingia ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Mufindi na Ikulu ndogo ya Wilaya ya Mufindi.
Msafara wa Rais Jakaya Kikwete ukiwa umesimama kwa muda eneo la Msitu wa Taifa wa Sao Hill Mufindi katika Barabara kuu ya Iringa- Mbeya kufuatia moto mkubwa kuwaka katika msitu huo mchana wa leo.
Kutokana na tukio hilo la moto msafara wa Rais Kikwete ulisimama na baada ya maofisa usalama kushuka na kutazama usalama zaidi wa msafara huo ndipo walioruhusu msafara huo kuendelea .
Askari Polisi akisimamisha msafara wa Rais Kikwete kutokana na moto mkubwa kutanda eneo hilo la Changalawe katika msitu wa Taifa wa Sao Hill umbali wa mita mbili kuelekea barabara ya Ikulu ndogo mjini Mafinga
Askari wa FFU wakishuka katika gari lao kwenda kuangalia usalama wa rais Kikwete na kulia gari la kwanza ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili la la tatu ni magari ya Ikulu yakiwa yamesimama.
Hata hivyo jitihada kubwa zilionekana kufanywa na kikosi cha askari wa JKT Mafinga pamoja na wananchi ambao walikuwa wakizima moto huo .Huku vyombo vya usafiri yakiwemo mabasi ya abiri yanayosafiri kutoka Dar es Salaam kuwenda mikoa ya kusini na nchi za kusini mwa Tanzania yakikwama kuendelea na safari kutoka na moto huo kushikakasi na moshi mzito kutanda barabara
Askari wakishuka kuingia katika moshi mzito kuangalia usalama wa rais katika eneo hilo ambalo moshi mzito ulitanda barabarani
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma alisema kuwa uongozi wa mkoa tayari umeagiza mkuu wa wilaya ya Mufindi kuwasaka waliohusika na uchomaji moto huo ili kuchukulia hatua kali.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mkoa wa Iringa umekuwa ukichukua hatua kali kwa wale wote wanaoanzisha moto kichaa kama huo hivyo kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi wahusika watasakwa popote walipo .
Msafara ukipita eneo hilo salama huku kulia ni askari wa JKT mafinga wakizima moto huo.
Mbali na hilo mkuu huyo amelipongeza jeshi la JTK Mafinga kwa kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na moto huo huku akisema madhara zaidi yatokanayo na moto huo yatatolewa baada ya moto huo kuthibitiwa .
Huu ndio moto unaoendelea kuteketeza msitu wa taifa wa Sao Hill Mufindi leo
0 comments :
Post a Comment