-->

AJITUPA KUTOKA GOROFANI BAADA YA KUJIFUNGUA

                 Dar es Salaam,Tanzania
MWANAMKE mmoja aliyejifungua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam, amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka Gorofani hadi chini,hata hivyo sababu za Mwanamke huyo kujiuwa hazijajulikana mara moja.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hussein Mwinyi, akifafanua jambo mbele ya vyombo vya habari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieth Mnangi, alisema kuwa mzazi huyo, Lewana Melkiory (38) mkazi wa Sinza, alijirusha kutoka wodi ya wazazi ghorofa ya pili juzi usiku na kufariki dunia papo hapo.  Alisema mwanamke huyo alijifungua Oktoba Mosi na kulazwa Hospitalini hapo na mtoto wake, maiti imehifadhiwa katika chumba cha maiti.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment