-->

WARAKA WAKUTISHA ULIONASIBISHWA NA UAMSHO WASAMBAA ZANZIBAR

 

Waraka wenye vitisho ukiwa na nembo ya Jumuiya ya
Uamsho na mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) umesambazwa visiwani Zanzibar, ukidaiwa kutishia kufanyika kwa shambulio dhidi ya viongozi wa dini na Serikali kabla ya Sikukuu ya Eid El Haj.


  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam amethibitisha kupata nakala ya waraka huo wenye maneno makali na vitisho kwa usalama wa watu na amani ya nchi. Kamanda
Mkadam alisema,Polisi imefanikiwa kuupata waraka huo baada ya tukio hilo kuripotiwa na baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini Visiwani humo. 

Hata hivyo, alisema,tayari makachero wa Polisi wako kazini na ametoa wito kwa viongozi wa dini na wananchi kuondoa hofu kwa vile vyombo hivyo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kukabiliana na tukio lolote la kihalifu.


Aliwasihi wananchi kuendelea na jitihada za kuwafichua wahalifu na watu wanaowatilia shaka dhidi ya amani visiwani hapa.


“Hatua tulizochukua ni pamoja na kuwataka viongozi
wa dini kuanzisha kamati za ulinzi mbali na kuwapatia huduma za ulinzi kama njia ya kukabiliana na matukio mbalimbali,”alisema Kamanda Mkadam.
Waraka huo unadaiwa kuainisha vitendo vya hujuma kuwa vitazidi hadi pale Zanzibar itakapofanikiwa kurejesha kile kilichoitwa Uhuru wake.

Source:
Gazeti la Mwananchi
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment