-->

UJERUMANI WAUTAKA UMOJA WA MATAIFA UICHUKULIE HATUA MAREKANI

Kansela Angela Merkel na rais Francois Hollande.

BAABA ya madai ya kudukukuliwa kwa simu ya mkononi ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na idara ya usalama wa Taifa ya Marekani NSA, washir
iki wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya wanataka hatua zichukuliwe.

Ingawa suala la ulinzi wa data na uendelezaji wa uchumi wa digitali lilikuwa miongoni mwa ajenda za mkutano mkuu wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels Ubelgji, hakuna aliejua kuwa lingepata umuhimu wa kipekee kabla ya mkutano huo.

Lakini sakata la udukuzi wa mawasiliano ya simu ya mkononi ya Kansela Angela Merkel limebadili mambo, na washiriki wa mkutano wanataka hatua zichukuliwe. 

Hadi jioni ya Jumatano, Ufaransa na Ujerumani zilikuwa na mitizamo tofauti juu ya taarifa kuwa idara ya Usalama wa taifa ya Marekani NSA ilikuwa imeyadukuwa mawasialiano ya raia wa Ulaya.

Barroso ailinganisha NSA na Stasi
Baada ya udukuzi huo kumgusa Kansela Merkel mwenyewe, kila kitu kilibadilika ghafla, na sasa Berlin na Paris zimeungana pamoja katika kuelezea kughadhabishwa na udukuzi huo. 


Rais wa halmashauri ya Ulaya Jose Manuel Barosso, alikwenda mbali na kuyiita tabia ya Marekani kuwa ni ya kiimla.
Rais wa Halmashauri ya Ulaya Jose Manuel Barroso. Rais wa Halmashauri ya Ulaya Jose Manuel Barroso.
"Tunafahamu hapa Ulaya nini maana ya utawala wa kiimla, na tunajua kinaochotokea pale serikali inapotumia madaraka yake kuingilia maisha ya watu. 

Kwa hivyo hili ni suala muhimu sana siyo kwa Ujerumani tu bali kwa Ulaya nzima - haki ya faragha, na ulinzi wa taarifa," alisema Barroso akiilinganisha NSA na shirika la ujasusi la iliyokuwa Ujerumani Magharibi.

Pia katika bunge la Ulaya, Kansela Merkel amepata uungwaji mkono na pia shinikizo, kutafakari juu ya athari za udukuzi wa mawasiliano si kwake tu bali pia kwa raia wote. Mbunge wa chama cha Kiliberali FDP Nadia Hirsh amemtaka Kansela Merkel kuonyesha sasa kuwa anawajali raia wake na siyo hadi yeye ageuke mwathirika ndiyo aonyeshe kujali.

Schulz: Mazungumzo ya biashara huru yasitishwe
Martin Schulz, ambaye ni rais wa Bunge la Ulaya na anaepewa nafasi ya kumrithi Barroso kama rais wa Halmashauri ya Ulaya, yeye ametaka hata mazungumzo juu ya makubaliano ya biashara huru kati ya Marekani na mataifa ya Ulaya yasitishwe kwanza.

"Mimi naamini sasa laazima kuwepo na wakati wa kusimama na kutafakari. 

Ninapokwenda kwenye mazungumzo na naanza kuhofia kuwa wenzangu katika upande wa pili, tayari wanajua kupitia ujasusi, kile ninachotaka kusema katika majadiliano, hapo kunakuwa hakuna usawa tena.
Rais wa Bunge la Ulaya Martin Schulz . Rais wa Bunge la Ulaya Martin Schulz.
 
Kwa hivyo naamini laazima kwanza tuzungumze na marafiki zetu Wamarekani juu ya viwango tunavyopaswa kulinda," alisema mwanasiasa huyo wa chama Social Democratic SPD cha hapa Ujerumani.

Siku ya Jumatano, saa chache kabla ya taarifa za udukuzi julikana, bunge la Ulaya, lilikuwa limepiga kura kusitisha mkataba wa mfumo unaojulikana kama SWIFT, ambao kupitia kwake, taarifa za kibenki za raia wa Ulaya hukabidhiwa kwa Marekani.

Lengo la mfumo huu ni kupambana na ugaidi, lakini wabunge wengi waliona kuwa unakiuka haki za faragha. 

Kabla ya sakata ka udukuzi kura dhidi ya mfumo wa SWIFT haikuwa na madhara makubwa kwa sababu serikali nyingi ambazi zinafaa kuridhia hatua hiyo, zinathamini zaidi suala la usalma kuliko udukuzi, lakini sasa upepo umebadilika kwa kiasi kikubwa.

Mada nyingine zafunikwa
Kabla ya matukio ya hivi karibuni, wengi walitarajia mkutano wa kawaida. Wakati wa mkutano huo, viongozi walitarajia kupiga hatua katika majadiliano ya kuedeleza muungano wa kichumi na kifedha inagawa hawakutemegea kufanya maamuzi yoyote ya msingi.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakiteta jambo wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja huo. Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakiteta jambo wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja huo.
 
Hata hivyo, suala la wakimbizi, ambalo Italia ililiweka katika ajenda ni la muhimu zaidi kuliko udukuzi, kwa sababu ni jambo la kufa na kupona kwa wahamiaji. 

Licha ya hivyo, hakutarajiwi kuwepo na mabadiliko makubwa katika sera ya wakimbizi ya Umoja wa Ulaya, kwa kuwa mataifa ya kaskazini hayataki kujihusisha na wakimbizi kabisaa.

Lakini kwa kulinganisha na maafa katika bahari ya Mediterranean, wakosoaji wanauona udukuzi wa Marekani kuwa ni jambo hafifu, hata kama simu ya Kansela wa Ujerumani ilidukuliwa. DW
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment