Mtandao
wa kijamii wa facebook una mpango wa kubadili sera yake ili kuwaruhusu
watumiaji wake kuweza kuweka picha ambazo zina maudhui ya kutisha ambapo
kama unakumbuka, May 2013 facebook ilipiga marufuku uonyeshwaji wa
picha za
matukio ya vurugu na mauaji pamoja na matukio yanayohusisha umwagaji wa damu na viungo vya mwili vilivyokatwa.
Sasa
hivi huo uamuzi unageuzwa japo hata hivyo facebook itaruhusu watu wenye
umri wa miaka 13 na kwenda mbele kujiunga na kuweka picha za matukio
kama haya lakini bado sera ya usalama ya facebook itaendelea kuzuia
picha zinazoonekana kutukuza vitendo kama hivi.
SOURCE:MILLARD AYO
0 comments :
Post a Comment