-->

KESI YA SHEKH PONDA YAUNGURUMA LEO HII,WAISLAM WAFIKA MAHAKAMANI BAADA YA SWALAT FAJIR

 http://4.bp.blogspot.com/-JrD4n19w2vo/UkqMlgw2H7I/AAAAAAAAKcI/f4j7O0sSVVE/s1600/IMG_4337.JPG


Leo tarehe 1/10/2013 ilisomwa tena kesi ya shekh ponda katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa Morogoro.Kama madai ya wakili wa Shekh Issa Ponda kwamba shitaka la kwanza la kushtakiwa kwenda kinyume na masharti aliyopewa katika mahakama ya kisutu basi shtaka hilo linapaswa kuendeshwa na mahakaam ya kisutu na sio katika mahakama ya mkazi mkoani Morogoro. Hivyo leo hii watu wengi walijaa mahakamani hapo ili kujua hatma ya kesi kwamba itaamishiwa Kisutu au itabakishwa Mkoani Morogoro.Kesi hiyo imeamuriwa kubaki mkoani Morogoro baada ya mjadala mrefu wa kisheria kati ya wakili wa Shekh Ponda na upande wa mashtaka.Kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 7 November mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza Mashahidi wa kesi hiyo.Sheikh Ponda Amerudiswa Rumande.
 Sheikh Issa Ponda akishuka kwenye basi la Magereza tayari KuingiaMahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro Kesi.
 Sheikh Issa Ponda Akiingia katika viwanja vya mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa morogoro.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment