-->

JUMA KASEJA ATEMWA KWENYE KIKOSI CHA TANZANIA BARA(KILIMANJARO STARS)

Juma Kaseja ametemwa kwenye kikosi cha timu ya Tanzania bara(Kilimanjaro Stars)kitakachoshiliki michuano ya Chalenji.Sababu ya kuachwa kwake ni kutokuwa na timu hivyo nafasi yake imechukuliwa na mlinda mlango wa Yanga sports club,na kifuatacho ndio kikosi cha Tanzania bara(Kilimanjaro Stars)
Wachezaji 16 wa kikosi cha Taifa Stars kitakachoingia kambini Novemba 12 mwaka huu kinaundwa na Ally Mustafa (Yanga), Mwadini Ali (Azam), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Nadir Haroub (Yanga).
Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na John Bocco (Azam).
Wachezaji wengine kumi kutoka Future Young Taifa Stars baadaye wataongezwa katika kikosi kitakachounda timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment