Na Oscar Assenga,Kilindi.
Askari
wa Mgambo wa Kijiji cha Lwande Wilayani hapa, Salum Mgonje amekufa kwa
kushambuliwa na mapanga na kundi la watuwaliokuwa wakipinga kitendo cha
mwenzao kulipishwa ushuru wa manunuzi ya zao la hiliki wa Serikali ya
Kijiji.
Mashambulizi hayo baadaye yalizusha mapigano baina ya kundi la
watu waliokuwa wakimsaidia mfanyabiashara huyo na askari wa jeshi la
polisi walipokwenda kuwakamata waliohusika na mauaji ya mgambo.
Katika mapigano hayo,Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kilindi
Edward Lusekelo, ambaye aliongoza askari waliokwenda kuwakamata wahusika
na mauaji ya Mgambo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi kwa bunduki
ya ShortGun.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamnada
wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Constantine Massawe, zilithibitisha kuwa
askari wa mgambo mmoja aliuawa juzi mchana katika tukio hilo lililotokea
katika kijiji cha Lwande, huku Mkuu wa kituo akijeruhiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi,Selemani Liwowa alisema chanzo cha
mapigano hayo ni mfanyabiashara huyo kutoka Kijiji cha Lulago Kata ya
Lwande kwenda Kijiji cha Lwande kununua hiliki ambapo baada ya kukaidi
kulipa ushuru mgambo alilazimika kumtia msukosuko ili aweze kulipa
kama ilivyo sheria ya kijiji.
Ndiyo chanzo cha kutokea kwa vurugu hizo baina mgambo na wafanyabiashara
ambapo baadaye walimshambulia kwa mapanga na kisha kumuua.
Aidha, alisema taarifa za mauaji ya mgambo zilizpofika kituo cha
Polisi ilimlazimu mkuu wa kituo kuongoza kikosi kilichokwenda kijiji
cha Lwande kwa ajili ya kuwasaka waliohusika na baada ya kuwasili
kijijini hapo likajitokeza kundi la watu wenye silaha na kuanza
kuwashambulia askari hao jambo lililosababisha askari hao kujibu
mashambulizi.
Akithibitisha
habari hizi,Kamanda Massawe alisema tayari watu wanne wanashikiliwa na
jeshi la Polisi kwa kuhusika na tukio hilo huku mkuu wa kituo cha
Polisi akiwa amekimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo kwa
ajili matibabu
CHANZO:MATUKIO NA MICHAPO
0 comments :
Post a Comment