TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Idara ya Habari – MAELEZO, inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania
kwamba Mheshiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo amepokea maombi kutoka kwa wamiliki wa Magazeti ya
Mwananchi na Mtanzania wakiomba kupunguziwa adhabu au kusamehewa adhabu
wanazozitumikia kuanzia 27 Septemba, 2013.
Wakati Mheshiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
anatafakari maombi hayo, amesikitishwa kuona kwamba magazeti haya mawili
yamekiuka masharti ya adhabu walizopewa.
Wamiliki wa Gazeti la Mtanzania
baada ya kufungiwa wameamua kuligeuza gazeti la kila wiki la RAI kuwa
la kila siku bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti. Kwa mujibu wa
ratiba ,gazeti la RAI linapaswa kutoka kila siku ya Alhamisi.
Wamiliki wa gazeti la Mwananchi nao wameendelea kuchapisha gazeti hilo katika mtandao kinyume na agizo la kufungiwa.
Serikali inawataka wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuwa na utamaduni
wa kutii sheria za vyombo vya habari zinazotumika wakati huu. Hivyo
serikali kwa mara nyingine tena inawataka wamiliki wa Gazeti la
MTANZANIA, kuzingatia ratiba yao ya kutoa gazeti lao kila siku ya
ALHAMISI.
Aidha, serikali inawataka wamiliki wa Gazeti la Mwananchi kuacha mara
moja kuchapisha gazeti lao katika mtandao kama amri ya kufungiwa
ilivyoanisha.
Imetolewa na,
Idara ya Habari – MAELEZO
10 Oktoba, 2013Idara ya Habari – MAELEZO
Blogger Comment
Facebook Comment