-->

ZITTO KABWE ASTAAJABU NG'OMBE NA BINAADAMU KUNYWA MAJI KISIMA KIMOJA HUKO KITUNDA

KATIKA POST YA MHESHIWA ZITTO KWENYE ACCOUNT YAKE YA FACEBOOK AMEPOST HABARI IFUATAYO AMBAYO IMEJAA JAA SIMANZI KUBWA NA YENYE KUSTAAJABISHA
 
Siku ya Nne ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetupeleka Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora.

Nikiwa na Wenyeviti wa chama wa mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora pia Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi Ndg. Mambo tumefanya mikutano 4.

MAJI

Kata ya Kitunda nilivunjika moyo sana baada ya kushuhudia wananchi wakichota maji ya Kunywa kwenye dimbwi ambamo Ng’ombe anakunywa maji. Maji yana rangi kama chai ya maziwa. Nimevunjika moyo sana sababu kwa umri huu wa Taifa letu Maji safi na salama haipaswi kuwa ni jambo la kukampenia tena au kufanyia siasa. Kina mama wanatembea kilometa nyingi kwenda kuchimba maji kwenye madimbwi. Watanzania hawastahili kabisa maisha ya namna hii. Nimepata uchungu sana sababu hizi ndio kazi wanasiasa tunapasa kufanya kusaidia wananchi na kwa kweli kukutana na hali kama hii kunavunja moyo sana.

Baadhi ya Wabunge tulisimama kidete kuhakikisha bajeti ya Wizara ya Maji inaongezwa na ikaongezwa TZS185 bilioni kwa ajili ya Maji vijijini. Ni wajibu wetu wabunge kuhakikisha fedha hii inafika kwa wananchi ili kuwaondolea madhila haya wasiostahili. Changamoto kama hizi za wananchi masikini wa vijijini zinanifanya nifikirie sana nafasi yangu binafsi katika siasa za nchi yetu, siasa za masuala na majawabu.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment