-->

RAIS WA CAMEROON PAUL BIYA AMPIGIA GOTI ETO'O KUTOSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA

Rais wa Cameroon Paul Biya amemshawishi mwanasoka Samuel Eto'o kutafakari upya mipango yake ya kujizulu kutoka soka ya kimataifa

Mshambulizi huyo wa Chelsea alikutana na waakilishi wa Rais mjini Yaounde kujadili mustakabali wa mchezaji huyo kuhusu soka ya kimataifa.

Sasa atakwenda Ufaransa kujiunga na timu ya taifa inayojiandaa kucheza dhidi ya Tunisia katika michuano ya kufuzu kwa kombe la Dunia Brazil mwaka 2014. Baada ya kukutana na Eto'o, alikubali kuchezea Cameroon kwa mara nyingine.

Etoo mwenye umri wa miaka 32 aliwambia wenzake kuwa hatacheza tena soka ya nyumbani punde tu baada ya Cameroon kuicharaza Libya na kuingia katika awamu ya pili ya kufuzu kwa kombe la dunia.

Licha ya ripoti za yeye kuacha kucheza soka, kocha wa timu ya Cameroon Volker Finke alimteua Eto'o kuchezea timu ya taifa ya Cameroon dhidi ya Tunisia ingawa mwenyewe hakuwa ametoa taarifa rasmi.

Eto'o amekuwa na uhusiano tete na maafisa wa soka nchini Cameroon katika siku za nyuma ikiwemo hata kuongoza timu ya taifa kwenye mgomo uliosambaratisha mechi ya kirafiki dhidi ya Algeria.

Eto’o aliadhibiwa kwa kupigwa marufuku kucheza mechi 15 ingawa baada ya kukata rufaa alipunguziwa adhabu hadi mechi 8

Hata baada ya adhabu yake kumalizika alikataa kuichezea Cameroon kwa miezi kadhaa.

Pia sio mara ya kwanza kwa Rais Biya kuingilia kati na kumzuia mchezaji kujiuzulu kutoka katika majukumu ya kitaifa.

Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment