Leo
October 26 2013 ndio Wanawake nchini Saudi Arabia wamepanga kuandamana
kupinga wao kunyimwa kuendesha magari sehemu yoyote nchini humo ikiwa ni
nchi pekee duniani ambayo inakataza Wanawake kuendesha magari hata kama
wanaweza.Unaambiwa
kwa sasa Mamlaka za Saudi Arabia zimewaonya Wanawake hao kutoandamana
katika maandamano hayo yatakayokua ya aina yake na ya tatu kutokea
nchini humo toka mwaka 1990 ambapo Wanawake kadhaa walikamatwa na
wengine kuachishwa kazi, onyo hilo linakwenda pia kwa Mwanamke yeyote
ambae amepanga kuendesha gariMsemaji
wa Serikali amesema Mwanamke yoyote atakae endesha gari leo
atachukuliwa hatua za kisheria ambapo wakati siku hii ya kuandamana
ikisubiriwa Wanawake kadhaa wa Saud Arabia tayari walishaweka video zao
wakiendesha magari sehemu mbalimbali za Saudia lakini mpaka sasa
hawajakamatwa.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment