-->

CHICHARITO SASA AFIKIRIA KUONDOKAMAN UNITED ILI AWEZE TIMIZA MALENGO YAKE

CHICHARITO AKIRI MUDA UMEFIKA ANAWEZA KUIHAMA UNITED

Javier Hernandez ametonya kwamba anaweza kuiacha klabu yake ya Manchester United ili afanikishe dhumuni lake la kuanza kucheza mara kwa mara, limeripoti Daily Mirror.
Straika huyo m-Mexico, ambaye anwindwa na Atletico Madrid, anasema anafuraha Old Trafford lakini, "najua ili nifanikishe lengo langu la kuanza mwanzo kila mechi mara kwa mara ni kuhamia klabu nyingine."

Mawazo ya FullSoka:
Inaeleweka kwamba kiuwezo Hernandez anastahili kucheza mara kwa mara - na ni dhahiri kuna klabu nyingin tu Premier League atakua akianza karibia mechi zote bila upinzani mkali - na mahojiano yake na kituo cha televisheni cha nchini kwao Mexico kiitwacho Deportes Telemundo yanatakiwa kua kama dalili mbaya na imshtue David Moyes - hasa aliposema: "Sasa najituma sana - ili nipate nafasi ya kua muhimu na kuanza. Najua wazi uwezo wangu dimbani unaniruhusu kufikia lengo hilo iwe hapa (United) ama mahali pengine nikichezea klabu nyingine."

United bado wanajitafuta baada ya Sir Fergie kuachia ngazi, Chicharito uwezo tunajua anao - ni haki aendelee kusubiri ama kama anavyodai yeye asipofanikiwa kutimiza lengo lake United basi aangalie ustaarabu mwingine?
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment