Kijana shekh sharif Khamis “16” ambae amekuwa kwenye kalama kubwa za
mwenyezi mungu kwa dua zake katika ya wiki hii amenusika kifo baada gari
yake kupata ajali mbaya kupelekea kuzunguka zaidi ya mara tatu na hali
yake sio nzuri kutokana na kuumia nyonga ya mguu wa kushoto.
Akiongea kwa shida kwa njia ya simu namba 0717-688792 Shekh sharif
alisema kuwa ajali hiyo iliwapata wakati wakitokea kijiji cha Mwailanje
kuelekea Kiteto Mkoani Arusha na wakiwa wanaelekea kwenye majukumu ya
kiimani huku gari hiyo ikiendeshwa na ustaadh Seif Othman na bila
kutarajia alitokea mtoto akiwa anaendesha baiskeli kwa kasi mbele yao na
dereva alipoona mtoto huyo anakaribia kuivaa gari kwa mbele ndipo
alipomkwepa.
Hata hivyo Shekh huyo aliongeza kusema baada ya dereva wake kufanikiwa
kumkwepa Yule mtoto ghafra upande uleule aliokwepea upande wa kushoto
tairi la mbele lilipasuka upande ambao alikua amekaa shekhe huyo.
Baada ya kupasuka tairi hilo gari hiyo lenye namba za usajili T283 AJZ
aina ya Lexus Aristi ilipoteza muelekeo na kupinduka zaidi ya ya mara
tatu kama inavyoonekana kwenye picha ambapo baada ya hapo watu wote
waliokuwemo ndani yake walitoka walipatwa na mshutuko huku shekh sharif
mwenyewe akiuumia vibaya.
Akiongea mara baada ya ajali hiyo shekh huyo ambae amekuwa nchini na
bara la afrika kwa ujumla kutokana mihadhara yake ya kuwaombea dua watu
na kabla ya kuelekea mkoani Arusha shekh huyo alikuwa kwenye ziara za
nchi za Burundi, Kongo, Angora na Zambia ambako huko alifanya mambo ya
kushangaza kwa dua zake kuziombea amani nchi hizo zenye migogoro ya
kivita.
Aidha katika hatua nyingine Shekh huyo mwanzoni mwa mwaka jana aliwahi
kupata ajali nyingine kama hiyo ambayo gari yake ilitumbukia kwenye
korongo na kukunjika kunjika kama chapati maeneo ya Morogoro lakini kwa
kudra za mwenyezi mungu alitoka salama.
Blogger Comment
Facebook Comment