-->

MAROUANE FELLAINI KUKAA NJE WIKI SABA

Fellaini nje wiki saba
Kiungo wa Manchester United, Marouane Fellani, ambae alisajiliwa kutoka Everton kwa adda ya pauni milioni 27, ameumia na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki saba, na huenda akafanyiwa upasuaji.
Mchezaji huyo hakuwemo katika kikosi cha United kilichoibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Sunderland FC, atakosa mchezo wa timu yake ya Taifa ya Ubelgiji wa kutafuta tiketi ya Brazili dhidi ya Croatia na Wales pia  michezo ya Ligi, Capital One na UEFA.Mchezaji wa mashetani wekundu analazimika kukaa nje ya mchezo kwa wiki saba baada ya kuumia kiwiko.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment