Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ametetea hatua ya nchi yake ya
kufanya operesheni za kijeshi katika nchi za Libya na Somalia. John
Kerry ambaye hivi sasa yuko kisiwani Bali huko Indonesia kwa ajili ya
kushiriki katika kikao cha Jumuiya ya Kiuchumi ya Asia na Pasifiki
(APEC) amesema hayo leo na kudai kuwa, Marekani haitaacha kampeni zake
za kupambana na makundi ya kigaidi. Vile vile waziri huyo wa mambo ya
nje wa Marekani amejigamba kuwa, wanachama wa mtandao wa al Qaida na
makundi mengine ya kigaidi wanaweza kukimbia, lakini kamwe hawawezi
kujificha. Hivi karibuni vikosi vya Marekani vilifanya mashambulizi
katika maeneo kadhaa ya Somalia na Libya kwa madai ya kupambana na
magaidi. Marekani inadai kuwa jana Jumamosi ilimtia mbaroni Abu Anas al
Liby, kiongozi wa ngazi za juu wa al Qaida kwa madai kuwa alihusika
katika operesheni za kushambulia balozi za Marekani katika nchi za Kenya
na Tanzania miaka 15 iliyopita. Katika shambulio jengine, vikosi vya
Marekani vimeua wanamgambo kadhaa wa ash Shabab nchini Somalia, baada ya
vikosi hivyo kuvamia makazi ya kamanda mmoja wa wanamgambo hao katika
mji wa Baraawe. Hata hivyo wanajeshi wa Marekani wameshindwa kumkamata
kamanda huyo wa ash Shabab.
HABARI KWA IHSANI YA:IRANI SWAHILI RADIO
HABARI KWA IHSANI YA:IRANI SWAHILI RADIO
Blogger Comment
Facebook Comment