ua vifaa vya kisasa vyenye matumizi rahisi katika soko la bidhaa hizo nchini.
Sony, inayoongoza pia katika soko la kimataifa ya vifaa vya Kielektroniki, imezindua Kamera tatu za kisasa na televisheni kubwa ‘Sony Bravia Full HD 3D LED TV W8 Series’.
Kamera zilizozinduliwa kwa lengo la kuleta mageuzi ya kiteknolojia nchini, ni Video Camera Sony Handycam HDR-PJ380 camcorder, Kamera ya picha za mnato Cyber-Shot HX300 digital still camera na runinga ya kisasa kwa matumizi ya nyumbani (Home Cinema System- BDV-N9900SH).
Akiongea wakati wa uzinduzi wa vifaa hivyo, mwakilishi wa Sony kwa nchi za Mashariki ya Kati na Afrika, Rajeev Pallippamadam alisema uzinduzi wa vifaa hivyo nchini Tanzania, unathibitisha dhamira ya Sony kuwekeza vifaa vya kisasa katika soko la Kielektroniki.
“Kama Kampuni, Tanzania ni moja ya kielelezo cha awali katika soko la vifaa vyetu. Leo tunataka kuwekeza uzoefu wa matumizi ya vifaa hivi, tukitegemea kuwa watumiaji watapata fursa nzuri na pana katika kutanua wigo wa uelewa wa vifaa vya Sony,” alisema Pallippamadam.
Uzinduzi wa vifaa hivyo ni sehemu ya mikakati ya Sony kujikita zaidi katika kuwekeza soko la vifaa vyake barani Afrika, ambapo imepanga kuongeza mtaji mara mbili kufikia Dola Bilioni 1.5 mpaka mwaka 2015.
Blogger Comment
Facebook Comment