Upinzani huko Ukrain umeapa kutotoka uwanja wa uhuru wanakoendeleza maandamano hayo.
Wakuu
kutoka umoja wa Ulaya wameshtumu vikali rais wa Ukrain Viktor
Yanukovych, kwa makabiliano makali baina ya polisi na waandamanaji
yanayoingia siku ya pili sasa .
Waziiri
Mkuu wa Poland , Donald Tusk, amesema atapendekeza Ukrain iwekewe
vikwazo vya kiuchumi huku yule wa Sweden Carl Bildt akiongeza kuwa damu
ya watu 25 waliokufa katika maandamano hayo iko mikononi mwa Yanukovych.
Vile vile wameutaka upinzani kuzuia machafuko zaidi ambayo yanasambaa kwengineko nchini humo.
0 comments :
Post a Comment