-->

PATA TASWIRA YA MECHI NZIMA KATI YA BUYERN MUNICH DHIDI YA ARSENA AMBAYO ILIISHA KWA ARSENAL KUPIGWA 2-0

Arsenal FC imepokea kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Bayern Munich katika  mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa Uwanja wa Emirates, London hivi punde. 
Arsenal waliokuwa nyumbani katika Uwanja wao wa Emirates wamemaliza mchezo wakiwa 10  baada ya kipa wao Wojciech Szczesny kumchezea rafu wimba wa Bayern Munich, Arjen Robben aliyekuwa anaelekea kufunga bao. 
Baada ya rafu hiyo, Szczesny alizawadiwa kadi nyekundu na kuamriwa ipigwe penalti langoni mwa Arsenal japo David Alaba  aliikosa. 
Mechi ya leo imeshuhudia timu zote mbili zikikosa penalti ambapo ya Arsenal imekoswa na Mesut Ozil na ya Munich ikikoswa na David Alaba.  Wafungaji mabao ya Munich walikuwa Toni Kroos na Tomas Muller. 
Hekaheka wakati wa mtanange huo.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment