Meneja Mradi wa SFCG wilaya ya
Tarime, Bwana Jacob Mulikuza, akielezea maudhui ya warsha ya namna ya
kuandika habari za migogoro kwa washiriki ambao ni waandishi wa redio za
jamii kutoka Tanzania, warsha hiyo inafanyika mjini Dodoma.
Washiriki wa warsha wakimsikiliza
Bw. Jacob Mulikuza kutoka Shirika la Search for Common Grounds – SFCG
(hayupo pichani) akielezea jambo wakati wa warsha ya namna ya kuandika
habari za migogoro inayoendelea mjini Dodoma kwa waandishi na
watangazaji wa Redio za Jamii nchini iliyofadhiliwa na UNESCO kupitia
mradi wa DEP.
Mmoja wa washiriki akifafanua jambo
katika warsha hiyo iliyojadili namna ya kuandika habari za migogoro
kutoka Shirika la Search for Common Grounds (SFCG) yanayoendelea mjini
Dodoma.
Mwezeshaji wa warsha hiyo ambaye pia
ni Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco, Mama Rose Haji Mwalimu,
akitoa utambulisho kwa waendesha warsha ya namna ya kuandika habari za
migogoro kutoka Shirika la Search for Common Grounds (SFCG),
yanayoendelea mjini Dodoma.
Meneja mradi wa SFCG wilaya ya
Tarime, Bwana Jacob Mulikuza, akiwapatia maelekezo washiriki wa warsha
ya namna ya kuandika habari za migogoro kuhusu namna ya uwajibikaji
katika kutatua migogoro ndani ya Jamii.
Mmoja wa washiriki Bwana Baraka
kutoka ORS Fm Radio, akiwaelezea washiriki wenzaka namna Ya kutatua
fumbo lililokuwa sehemu ya kazi za Vikundi, katika warsha ya Uandishi wa
habari za Migogoro kuhusu namna ya uwajibikaji katika kutatua migogoro
ndani ya Jamii.
Mratibu wa vyombo vya habari wa SFCG
Zanzibar, Bwana Ali sultan, akielezea kuhusu ushiriki wa SFCG huko
Zanzibar katika warsha ya namna ya kuandika habari za migogoro kwa
washiriki ambao ni waandishi wa Redio za Jamii kutoka Tanzania, warsha
hiyo inayofanyika mjini Dodoma imefadhiliwa na Shirika la UNESCO kupitia
mradi wa Demokrasia na Amani (DEP) kuelekea Uchaguzi 2015.
Meneja Mawasiliano wa SFCG kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Bwana Dupont Ntererwa, akielezea
kuhusu ushiriki wa SFCG huko DRC katika warsha ya namna ya kuandika
habari za migogoro kwa washiriki ambao ni Waandishi wa Redio za Jamii
kutoka Tanzania, warsha hiyo inayofanyika mjini Dodoma.
Washiriki wakifanya kazi za vikundi.
CHANZO:MJENGWA
0 comments :
Post a Comment