-->

WAZIRI WA FEDHA ASEMA SERIKALI HAINA MPANGO WA KUBADILI NJIA YA UKUSANYI WA KODI

saada a204d
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya amesema Serikali haina mpango wa kubadili ukusanyaji wa kodi kupitia mashine za elekroniki EFDS na kwamba, ipo tayari kupambana na wafanyabiashara wote wanaopingana na utaratibu huo.
Akizungumza kwenye mahafali ya Chuo cha Kodi (ITA), Waziri Mkuya alisema Serikali haitarudi nyuma kubadili utaratibu huo utakaosaidia kukusanya mapato kwa ufanisi, lengo likiwa ni kuwafurahisha wafanyabiashara wanaotaka kuvunja sheria.
Waziri Mkuya anasema Serikali inafahamu baadhi ya changamoto za mfumo huo, lakini ipo tayari kupokea mawazo kutoka kwa wadau mbalimbali ili yafanyiwe kazi inapobidi.
"Kamwe hatutarudi nyuma na kubadili mfumo huu, kama kuna watu wanataka kupingana na tupo tayari kupambana nao hatuwezi kuvumilia kuona sheria zinavunjwa," alisema Waziri Mkuya na kuongeza: "Tunapozungumzia maendeleo ya sayansi na teknolojia basi zitumike katika nyanja zote, hivyo hata biashara lazima twende kulingana na mabadiliko haya, changamoto haziwezi kutatuliwa kwa mgomo wala maandamano."
Pia, aliwataka wahitimu wa chuo hicho kutumia taaluma waliyopata kupambana na changamoto mbalimbali zinazokabili ukusanyaji mapato, ikiwamo ukwepaji kodi "Bado kuna tatizo la wafanyabiashara kukwepa kodi, vilevile wananchi wengi hawajui wajibu wao katika suala zima la ulipaji kodi ndiyo maana wanashindwa kudai risiti, matokeo yake wanawanufaisha wachache," alisema.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Profesa Palamagamba Kabudi aliwasihi wahitimu hao kufanya kazi kwa weledi, ufanisi na uaminifu kuisaidia Serikali kukusanya mapato yatakayosaidia uendeshaji. "Mnapaswa kwenda kufanya kazi kwa weledi, ufanisi na uaminifu tunatarajia elimu mliyopata itakuwa chachu ya maendeleo ya taifa hili," alisema.Chanzo: mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment