-->

MAN U HAIJAWAHI KUFUNGWA NA TIMU INAYOTOKA UGIRIKI,JE OLYMPICOS NAYO ITAFUNGWA?

man u fc5ad
Olympiakos wana matumaini ya kuharibu rekodi ya Manchester United FC dhidi ya timu za Ugiriki wakati watakapokutana katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League katika dimba la Stadio Georgios Karaiskakis.
• Mabingwa wa Uingereza hawahajwahi kupoteza mechi dhidi ya timu kutoka Ugiriki, lakini Olympiacos wapo kwenye kiwango kizuri na wanaweza kuiadhibu United..
Mechi zilizopita
• United wameshinda mechi zote nne zilizowahi kuwakutanisha na Olympiacos, ushindi wa kwanza ulikuwa 2-0 jijini Piraeus msimu wa 2001/02 katika mechi ya makundi, mabao ya David Beckham na Andrew Cole aliyefunga mawili. Kikosi cha Sir Alex Ferguson tena kikashinda 3-0 jijini Manchester Ole Gunnar Solskjær, Ryan Giggs na Ruud van Nistelrooy walifunga katika dakika 15 za mwisho. Roy Carroll, ambaye sasa anaichezea Olympiacos lakini hayumo katika kikosi cha UEFA Champions League, alikuwa benchi katika michezo yote miwili.

• Giggs amecheza mechi zote nne ambazo United imekutana na Olympiacos na kocha mchezaji huyo wa United, alikuja kufunga tena wakati United iliposhinda mabao 4-0 katika msimu wa 2002/03 kwenye makundi. Giggs alifunga mara mbili huku Solskjær na Juan Sebastián Verón nao waliziona nyavu.

• Olympiacos waliweza kuzigusa nyavu za United katika mchezo wa marudiano uliofanyika 23 October 2002. Wakiwa nyuma kwa mabao ya Laurent Blanc na Verón, Lampros Choutos na Predrag Djordjević wakaisawazishia Olympiacos lakini wakaja kufa dakika za mwisho na goli la Paul Scholes.

• Vikosi vilikuwa hivi:
Olympiacos: Eleftheropoulos, Anatolakis, Antzas, Venetidis, Patsatzoglou, Giannakopoulos (Mavrogenidis 87), Zetterberg (Ofori-Quaye 71), Karembeu, Djordjević, Giovanni (Choutos 46), Dracena.
Manchester United: Barthez, G Neville, Blanc, O'Shea, Silvestre, Beckham (Fortune 63), P Neville, Verón (Richardson 87), Giggs (Chadwick 63), Scholes, Forlán.

TAKWIMU
• Olympiacos wanatafuta ushindi wa 3 mfululizo katika dimba la nyumbani katika champiosn leahue msimu huu baada ya kushinda mechi dhidi ya Benfica na Anderlecht.

• United hawapoteza mechi msimu huu ugenini wakitoka sare na FC Shakhtar Donetsk na Real Sociedad de Fútbol na wakaifunga Bayer 04 Leverkusen 5-0 – katika ushindi wao wa mabao 5 katika UCL tangu mwaka 1965.

• Olympiacos wamepoteza mechi zao tano za hatua ya mtoano dhidi ya vilabu vya Uingereza katika michuano ya UCL. Hata hivyo, wameshinda mechi 3 nyumbani kwao dhidi ya timu za EPL - zote dhidi ya Arsenal.

• Rekodi ya Olympiacos dhidi ya vilabu vya EPLW5 D3 L3.
Habari za timu
Javier Saviola yupo nje kutokana kuwa na majeruhi ya paja aliyopata wikiendi, ingawa Nelson Valdez (enka) sasa amerudi. Giannis Maniatis, Iván Marcano, Delvin N'Dinga, Alejandro Domínguez na Michael Olaitan wote walipumzishwa jumamosi.
Jonny Evans (misuli) na Phil Jones hawajasafiri na timu kwenda Piraeus lakini wachezaji wote wameenda kasoro Juan Mata ambaye haruhusiwi kucheza michuano hii. Chanzo: shaffihdauda
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment