Nyota
wa kimataifa kwenye soka ambaye ni mchezaji mwenye umri wa miaka 53
kutoka Argentina Diego Maradona amekuwa katika mazungumzo na klabu ya
Deportivo Riestra, ambayo inashiriki ligi ya chini kabisa kwa lengo la
kujiunga nao kama mchezaji mpaka kumalizika kwa msimu.
Nchini kwake ni maarufu kwa jina ‘God’ Maradona amekuwa akipambana
na uzito katika siku za hivi karibuni kwa lengo kujiweka sawa na fiti
kabla ya kuanza mchezo wake wa kwanza March 23.
Mmoja wa wachezaji wa Deportivo Kiungo Victor More, amesema yuko
tayari kuvua jezi yake nambari 10 anayova sasa na kumkabidhi Maradona
atakapo saini kuichezea klabu hiyo na pengine mkongwe huyo anayetumia
mguu wa kushoto akarejea kuitendea haki jezi hiyo aliyokuwa akiivaa enzi
zake
0 comments :
Post a Comment