
Assalaamu Alaykum. Hivi ulishawahi kutafakari kwa kina kwanini elimu
tanzania inashuka kila wakati. Zipo sababu nyingi ila na mtaala
unachangia kiasi fulani. Rejea mtaala wa sekondari (2007). Mwaka una
siku (365), siku za mwanafunzi kuwa shule (194) tukitoa weekend (siku
138.57) ambazo ni sawasawa na majuma 19.79 ukilinganisha na majuma 52
kwa mwaka. Mwanafunzi anatakiwa kusoma vipindi visivyopungua 40 kwa wiki
na kila kipindi kiwe na dakika 40. Hivyo mwanafunzi anasoma masaa
527.73 kwa mwaka ukilinganisha na jumla ya masaa 8760 ya mwaka.
Hitimisho kwenye mabano ndo hali halisi inayotakiwa kutendeka kwa
mujibu wa data hizo hapo juu. mwaka 365 (138.57), miezi 12 (4.6), majuma
52(19.79), masaa 8760 (527.73) ambayo ni asilimia 6.02% ya maisha ya
mwanafunzi kwa mwaka. Kwa hali hii unategemea nini? Chanzo NECTA tangu
mwaka 2007 mpaka 2012 ni asilimia 14.33% waliofahuru kwa daraja la
kwanza mpaka la tatu (yaani waliobatika kuendelea). Haya walimu kazi
tunayo tufanyeje?
SOURCE:FB(NASHIR KAMUGISHA)
0 comments :
Post a Comment