JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
TAARIFA KWA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA_______________________________________________
Kufuatia
wito wa Serikali kuwa Wajumbe wote wanaombwa kufika Mjini Dodoma
kuanzia tarehe 16 Februari, 2014 katika Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu
wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar wanapenda kuwaarifu Wajumbe wote
maandalizi yafuatayo: -
1.0 USAFIRI WA KUFIKA DODOMA
Wajumbe
wote wanatakiwa kujigharamia wenyewe kufika Dodoma kwa vyombo vya
usafiri wa umma. Wajumbe watarejeshewa gharama za usafiri wa kufika
Dodoma kutoka maeneo wanayotoka baada ya kuwasilisha stakabadhi za
gharama walizotumia kwa usafiri.
2.0 MALAZI
Utaratibu
wa malazi umeandaliwa. Hoteli zilizoteuliwa kwa malazi kwa Wajumbe
kuchagua kwa kadri itakavyowapendeza zimeainishwa. Hoteli hizo ni hizi
zifuatazo: -
NA.
|
JINA LA HOTELI NA MAHALI ILIPO
|
IDADI YA VYUMBA
|
MAWASILIANO
| |
1.
|
Dodoma Hotel - Mjini
|
87
|
0262321641
0262353782
| |
2.
|
St Gaspar Conference Centre - Kisasa
|
73
|
026235226
0767999903
| |
3.
|
Hotel Fifty Six - Viwandani
|
53
|
0757202630
0713702066
| |
4.
|
Four Points Hotel - Kisasa
|
20
|
026 2350214
0757 613270
| |
5.
|
Peter Palm Hotel
|
22
|
0767888311
0784888311
| |
6.
|
Cana Lodge - Mjini Barabara ya 9
|
17
|
026 2321199
0713 786611
| |
7.
|
Dodoma Grand Hotel - Majengo
|
20
|
026 2321187
|
NA.
|
JINA LA HOTELI NA MAHALI ILIPO
|
IDADI YA VYUMBA
|
MAWASILIANO
|
8.
|
Kingstone Lodge
|
17
|
026 2323057
|
9.
|
Hotel DM - Majengo
|
19
|
0712 447325
|
10.
|
Golden Glory Guest House - Area C
|
11
|
026 2353343
|
11.
|
Modern Hotel - Area C
|
35
|
026 2304466
|
12.
|
Nam Hotel - Area C
|
28
|
0756 652659
026 2354467
|
13.
|
Marryland Hotel - Area C
|
20
|
0757 919166
|
19.
|
Giftland Hotel - Area C
|
48
|
0762 159099
|
20.
|
Golden Crown Hotel - Area C
|
27
|
0757 760333
|
21.
|
Joanic Hotel - Kisasa
|
33
|
0653 867026
|
22.
|
Kidia Vision Hotel - Mji Mpya
|
47
|
0262320095
0784520192
|
23.
|
VETA Hotel
|
12
|
0756 698408
|
24.
|
Area D Lodge - Area D
|
8
|
0764 698408
|
25.
|
Formula One - Makole
|
8
|
0755 404621
|
26.
|
Summit Hotel - Ipagala
|
42
|
0715 816000
|
27.
|
Kitemba Hotel - Oneway
|
24
|
026 2323578
|
Wajumbe watalipwa posho ya kujikimu na watalazimika kujitegemea kwa gharama za malazi katika hoteli watakazofikia.
1.0 USAJILI
Zoezi la
Usajili litafanyika kwenye Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma kuanzia Saa Tatu
Asubuhi tarehe 16 Februari, 2014 hadi tarehe 17 Februari, 2014.
Zoezi
hilo litajumuisha Ujazaji wa Fomu ya Usajili, Upigwaji Picha za
Vitambulisho na Kukabidhiwa Begi lenye maelezo muhimu na stahiki
nyinginezo kama zitakavyoainishwa.
Wajumbe wote wanapaswa kufika na nakala halisi ya vitambulisho vyao ili waweze kutambuliwa kwa usajili.
Vitambulisho vitakavyokubalika ni: -
(i) Shahada ya Kupigia Kura;
(ii) Kitambulisho cha Taifa;
(iii) Kitambulisho cha Zanzibar;
(iv) Hati ya Kusafiria;
(v) Leseni ya Kuendeshea gari;
(vi) Kitambulisho cha Mwajiri anayetambulika.
Iwapo
Mjumbe hana kitambulisho chochote kilichoainishwa hapo juu basi anaombwa
kuwasiliana na Maofisa waliotajwa katika Tangazo hili ili kuona namna
anavyoweza kusaidiwa.
1.0 MKUTANO WA MAELEKEZO YA AWALI
Katibu wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu wa Baraza la
Wawakilishi wameandaa Mkutano wa Maelekezo ya awali siku ya Jumatatu
tarehe 17 Februari, 2014 kuanzia Saa Kumi Jioni.
Wajumbe
wote wanapaswa kuhudhuria Mkutano huo bila kukosa ambao utajumuisha
utaratibu wa ukaaji, jiografia ya viwanja vya Bunge na huduma za
utawala.
1.0 SHUGHULI ZA KIKAO CHA KWANZA
Kikao cha
Kwanza kitafanyika Siku ya Jumanne, tarehe 18 Februari, 2014 ambacho
kitajumuisha Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda atakayesimamia upitishwaji
wa Kanuni na Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
2.0 MAWASILIANO
Kwa taarifa zaidi, Wajumbe wanaombwa kuwasiliana na:
Ofisi ya Bunge Maalum,
S. L. P. 901,
DODOMA.
Simu: 026 23 22 696
Fax: 026 23 23 116
Aidha, Wajumbe wanaweza kupata ufafanuzi zaidi kutoka kwa Maafisa wafuatao:-
1. Ndg. John Joel
(0754 260 831)
2. Ndg. Amour Amour
(0777 855 878)
3. Ndg. Kitolina Kippa
(0754 363 237)
4. Ndg. Saidi Yakubu
(0762 089 225)
5. Ndg. Abdu Haji
(0779 894 847)
6. Ndg. Mossy Lukuvi
(0767 401 333)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU WA BUNGE NA KATIBU WA BARAZA LA WAWAKILISHI
15 FEBRUARI, 2014
0 comments :
Post a Comment